Waziri Bashe atangaza neema Sekta ya Umwagiliaji Shinyanga

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe ametembelea mradi wa Umwagiliaji wa Nyida uliopo mkoani Shinyanga wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kuelekeza kuwa ndani ya mradi huo lijengwe ghala kubwa la kuhifadhi mpunga.

Waziri Bashe pia ameelekeza ufanyike ujenzi wa kituo  cha pamoja cha kununua mpunga na kufungwa mashine na kinu cha kuchakata mchele,sanjari na ujenzi wa barabara ya uhakika yenye urefu wa km 7.5 itayoungana na barabara kubwa ya lami na kujenga pamoja na kujenga Mabirika ya kunyweshea wanyama.

Waziri Bashe amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua Ujenzi wa mradi wa Umwagiliaji wa Nyida uliopo mkoani Shinyanga. 

Aidha Waziri Bashe amebainisha dhamira ya serikali ya kuongeza mradi mdogo wa Nyida utakaokuwa na zaidi ya hekta 400 na ambapo ujenzi skimu hiyo utatangazwa hivi karibuni. 

“Mradi huu ni ndoto za muda mrefu nilikuja mwaka 2020 na  leo namshukuru Mungu tumekuja hapa kuangalia maendeleo,namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia  Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha,mradi huu utakuwa na mabwawa matatu na ujenzi wa skimu nyingine ya Lyamalagwa yenye  hekta 1500 ikiwa na mfereji mkuu km 12 na mifereji ya ndani yenye zaidi ya kilometa 50,”alisema.

Amesema ujenzi wa miradi hiyo iliyoanza Nyida pekee serikali inatumia fedha za walipa kodi zaidi ya shilingi billioni 55 na kuelekeza ujenzi huo ufanyike kwa kiwango kinachotarajiwa na utunzwe kwa maslahi ya wananchi wa Shinyanga na Taifa kwa ujumla

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa, amesema kuwa Tume hiyo inaendelea na mpango wa kujenga mabwawa, kukarabati skimu za zamani na kuibua maeneo mapya kwa ajili ya kilimo cha Umwagiliaji. 

“Mkoa wa Shinyanga una jumla ya skimu 14, sikimu nyingi zilijengwa muda mrefu na hivyo kuwa chakavu na nyingine kutokamilika ikiwemo Ishololo, Mwamashele, na Kahanga,”alisema.

Mndolwa amesema ujenzi wa bwawa  la Nyida ulianza mwaka 2023 na unatarajiwa kukamilika April mwakani ambapo hadi sasa umefikia asilimia 68.

Miradi mingine inayotekelezwa na Tu me hiyo ni ujenzi wa mabwawa ya Katunguru Sengerema Mwanza na Kasoli,Bariadi Simiyu yote matatu yakiwa na gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 29.

Aidha kwa mwaka wa fedha 2024/2025 serikali kupitia Tume imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mabwawa saba  na katika mabonde ya Lunguya, Mwamkanga, Amani, Ngaganulwa, Nimbo, Bulungwa na Kisuke.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top