Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Je Unafahamu Kuwa Unaweza Kutumia Pump za Umwagiliaji Zinazotumia Solar Zinazohamishika Kumwagilia Shamba Zaidi ya Moja Kwa Gharama Nafuu?

 


Na Emmanuel Chibasa

Katika maeneo ya vijijini mkoani Mara, wakulima wanakumbana na changamoto katika kilimo Cha umwagiliaji kutokana na kukosa elimu ya matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kutengeneza mifumo ya nishati ya jua (Solar) unaohamishika Ili kupunguza gharama za uendeshaji wanazotumia Katika pump za mafuta.

Uchunguzi uliofanywa George Marato Tv katika baadhi ya maeneo Musoma umebaini kuwa  wakulima wanatumia pamp za mafuta ambazo wanaweza kumwagilia Kwa kuhamisha lakini hawana uelewa kuwa Kuna teknolojia ya mfumo wa pump za umwagiliaji Zinazotumia solar zinazohamishika na hivyo kuwa ni Suluhu mbadala ya kupunguza gharama wanazotumia Katika pump za mafuta lakini pia kuhifadhi mazao baada ya mavuno Ili yasiharibike.

Wakulima pia hawana uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya Teknolojia ya umeme jua inauwezo WA Kuongeza uzalishaji na kupunguza upotevu WA mazao baada ya mavuno na Kuboresha Maisha ya wakulima na Uchumi wa nchi Kwa ujumla na teknolojia hii inaweza Kuleta mabadiriko chanya Katika Taifa 

Tayari baadhi ya taasisi hapa nchini zimeanzisha suluhisho la kipekee kubadilisha kilimo katika maeneo ya vijijini  kwa kutumia pampu za umwagiliaji za nishati ya jua zinazohamishika.

Mhandisi Adrian Edwin Mapunda ni mtaalam wa nishati ya umeme jua kutoka shirika hilo, anasema asilimia 83 ya maeneo yanayolimwa hapa nchini yanalimwa na wakulima wadogo na wamekua wakiwasaidia wakulima katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji na wanatekeleza mpango wa kusambaza mifumo ya umwagiliaji ya jua inayohamishika na grid ndogo za umeme zinazohusiana na kilimo katika maeneo ya vijijini.

Mfumo wetu wa kisasa wa pampu za maji za umeme wa jua wenye uwezo wa 0.5 – 2 hp, unaoendeshwa na moduli za PV za 600W – 1,200W zilizowekwa kwenye trolly ya jua, una uwezo wa kupump maji hadi lita 20,000 kwa siku kwa umbali wa hadi 0.8km. Kwa kubadilisha pampu za mafuta ya petroli ambazo ni ghali na zinahitaji matengenezo mengi, mifumo ya umwagiliaji ya jua ya ELICO inatoa mbadala wa kimsingi na wenye ufanisi unaolingana na mahitaji ya wakulima wadogo.

Akielezea juu jinsi teknolojia hiyo inavyoweza kubadilisha kilimo katika maeneo ya vijijini amesema  pampu za umwagiliaji zinazotumia nishati ya jua inayohamishika inatoa suluhisho bora kwa wakulima wa vijijini Kwa kutumia moduli za PV zilizowekwa kwenye troli, wakulima wanaweza kubeba pampu hizi kutoka eneo moja hadi lingine, hivyo kuongeza ufanisi wa umwagiliaji. Tunatumia mifano ya umiliki, upangaji, na matengenezo ili kuhakikisha kwamba teknolojia hii inakuwa rahisi kupatikana na nafuu kwa wakulima.

“Kwa kubadilisha pampu za mafuta ya petroli ambazo ni ghali na zinahitaji matengenezo mengi, mifumo ya umwagiliaji ya jua ya ELICO inatoa mbadala wa kimsingi na wenye ufanisi unaolingana na mahitaji ya wakulima wadogo.

Pia kuwawezesha wakulima wadogo kupata zana wanazohitaji kustawi. Mkakati wa usambazaji unajumuisha mfumo wa PAY-AS-YOU-GO kwa umiliki, umwagiliaji kama huduma, pamoja na mitindo ya upangaji inayowezesha wamiliki kupata mapato huku ikihimiza matumizi ya kijamii.” Amesema Mhandisi Adrian


Teknolojia ya matumizi ya nishati ya umeme jua inayohamishika inonekana  bado haijafahamika kwa wakulima wengi kutokna na kukosa elimu ya namna wnavyoweza kuitumia katika shughuli zao za kilimo na hivyo kuondokana na matumizi ya pampu za mafuta ambazo huzitumia kwa kuhamisha kutoka eneo moja kwenda jingine.

Moja ya mkulima Chacha Mang’era  kutoka Musoma, akizungumza na George Marato Tv katika mahojiano maalum ameonesha  kushangaa aliposikia  kuhusu teknolojia hii katika mfumo matumizi ya umeme wa solar zinavyoweza kuhamishika katika kilimo cha umwagiliaji maji kutoka sehemu moja hadi nyingine .

“Nilikuwa sijasikia kuhusu hili kabla na nilidhani umwagiliaji wakutumia  Solar unahitaji vifaa vya kudumu vilinavyungwa sehemu moja hususasni juu ya bati, na sikujua kuwa kuna njia rahisi ya kubeba vifaa hivyo kutoka shamba moja hadi lingine.” Amesema Chacha

Naye Mwasi  Zebedayo  ambaye pia ni mkazi wa Musoma amesema  ameona pampu za umwagiliaji zinazotumia solar zinazohamishika zina faida nyingi kwa  kufanya kazi katika maeneo tofauti, siyo lazima ziwe sehemu moja  hivyo mkulima  haituhitaji mafuta na wataalamu wanasema  matengenezo machache na hii inamanisha wakulima wanaweza kutumia maji kwa ufanisi zaidi na kupunguza gharama.”

Kwa upande wake Francis Mtayomba  kutoka rusoli musoma vijijini amesema wakulima hasa walio kwenye vikundi wanapaswa kufikishiwa elimu hii kwa wingi ili kuwasaidia kutatua changamoto katika kilimo cha umwagiliaji.

 “Sikujua kwamba tungeweza kutumia pampu hizi kwa kuhamisha na kutumia kwa pamoja, Tukijipanga na kupata uelewa zaidi vikundi vyetu vinaweza kushirikiana kununua na kutumia pampu hizi, hivyo kusaidia kumwagilia mashamba ya wanakikundi wote kwa pamoja na kuongeza uzalishaji” Amesema Francis

Wakulima kutoka musoma na maeneo mengine ya mkoa wa Mara wakitumia nishati ya umeme wa Solar kwa kutengeza mfumo unao hamishika na wakulima wakijengewa  uelewa wakutosha juu ya matumizi teknolojia hii wataweza kufaidika kwa njia bora zaidi na kuboresha uzalishaji wa mazao yao na hivyo kukabiliana na athari za mabadiriko ya tabia nchi pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wanazotumia katika matumizi ya pump za mafuta pamoja na mazao kuharibika baada ya mavuno

Licha ya serikali ya Tanzania kusisitiza matumizi ya nishati safi Ili Kulinda afya za Watanzania lakini Sekta ya kilimo bado  inaonekana kuachwa nyuma licha ya kuwepo rasilimali jua ambapo  sababu  Kuu ikitajwa kuwa ni uelewa mdogo wa matumizi ya nishati ya umeme jua huku vyombo vya habari na Waandishi wa habari wakidaiwa kuwa na mchango mdogo Katika Kutoa habari na kuelimisha Jamii juu ya faida ya nishati hiyo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kituo Cha ubora wa Vyombo Vya habari Africa(ACME) uliofanywa Mwaka 2023 kuhusu uandishi wa habari za nishati ya umeme jua Katika kilimo Katika nchi za Africa mashariki unaonesha kuwa Katika sampuli ya habari 63 waliochukua kwenye Vyombo Vya habari maarufu Katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda unaonesha Kati ya Vyombo hivyo, Vyombo vya habari kutoka Uganda viliandika habari 30, Kenya 23 huku Tanzania Ikiwa na habari 10 na Kati ya habari hizo zilizotolewa kwenye luninga ni 33 huku habari zilizotolewa kwenye magazeti zikiwa 29.

Katika bajeti ya wizara ya kilimo ya Mwaka 2023/2024 serikali imeweka Mkakati wa Kujenga mabwawa 100 nchi nzima Yenye Uwezo wa kuhifadhi Lita Bilioni 900 nchi nzima na Kwa Mkoa wa Mara serikali inatarajia Kujenga Miundombinu ya umwagiliaji Katika bonde la Bugwema na Suguti Katika Halmashauri ya Musoma Vijijini baada ya hatua ya hatua ya upembuzi yakinifu kukamilika.

Wakulima Mkoani Mara wakitumia fursa hii ya Mradi wa kilimo Cha umwagiliaji Kwa Kutumia teknolojia ya umeme jua Katika kilimo Cha umwagiliaji, Uhifadhi wa mazao ya chakula Ili yasiharibike baada ya mavuno pamoja wataweza kukuza Uchumi, kuwa na Usalama wa chakula pamoja na Utunzaji wa Mazingira.

Picha zote na Maelezo ya Mtaalam ni kwa hisani ya Elico Foundation.


Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...