Serikali imewaahidi vijana nchini kuwasikiliza na kuyafanyia kazi mahitaji yao ikiwemo la ajira na mitaji ili kuwawezesha kundi hilo kufanya biashara na shughuli nyengine za kiuchumi na hivyo kuwezesha kuongeza kipato Chao.
Ahadi hiyo kubwa imetolewa Jijini Dodoma na waziri ofisi ya waziri mkuu,anayeshughulikia, kazi,ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Ridhwani Kikwete kwenye kongamano la Vijana lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali inayoitwa #DOYODO ikishirikiana na wadau mbalimbali.
Mhe. Kikwete ametumia Jukwaa hilo kuwaeleza vijana juu ya nia ya serikali kuendelea kuwahudumia vijana katika maeneo mbalimbali ya maisha yao na utayari wake wa kukutana nao.
Amesema uamuzi wa kukutana na vijana hao katika ngazi za chini za maamuzi zinalenga kukabili changamoto walizonazo kupitia programu mbalimbali zinazoendeshwa pamoja na marekebisho na sera na sheria ili ziendane na mahitaji yao ya sasa.
Kongamano hilo kubwa limeshirikisha vijanan 632 kutoka mikoa yote nchini.






Comments
Post a Comment