Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

NIRC YALETA MAPINDUZI YA UMWAGILIAJI KWA WAKULIMA NA VIJANA

  Na Mwandishi Wetu, Dodoma Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imetangaza kuanza kwa utekelezaji wa miradi mipya zaidi ya 30 ya umwagiliaji katika mwaka wa fedha 2026/2027, sambamba na mpango wa kugawa zaidi ya pampu 2,000 za umwagiliaji na kuajiri kati ya vijana 2,000 hadi 4,000 kupitia miradi ya uchimbaji wa visima nchini. Hatua hiyo inalenga kuongeza uzalishaji wa mazao, kupunguza utegemezi wa mvua na kuimarisha mchango wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Malecela jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Raymond Mndolwa, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha wakulima wanapata miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji ili kuongeza tija katika uzalishaji. "Lengo letu ni kuhakikisha mkulima wa Tanzania anazalisha kwa tija mwaka mzima bila kutegemea mvua. Umwagiliaji ni msingi wa kilimo cha kisasa na chenye tija," alisema Mndolwa. Alis...

NEEMA KILINDI: DARAJA LA MILIONI 923 KUMALIZA KERO YA MAWASILIANO, MNEC AAGIZA WAKANDARASI WALIPWE

 Na Mashaka Mhando, KILINDI KERO ya muda mrefu ya kukatika kwa mawasiliano nyakati za mvua kwa wananchi wa Mgera wilayani Kilindi inatarajiwa kubaki historia, kufuatia ujenzi wa Daraja la Mgera unaogharimu Shilingi Milioni 923 unaolenga kuwawezesha wananchi kufikia huduma za msingi kwa urahisi. Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Mohammed Salim 'Ratco', wakati Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tanga ilipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM. Ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuleta tija iliyokusudiwa, MNEC Ratco alitoa agizo zito kwa viongozi wa Wilaya kuhakikisha wakandarasi wanalipwa fedha zao kwa mujibu wa mikataba. "Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa Halmashauri, suala la kuwalipa wakandarasi kwa wakati ni wajibu wetu. Lazima tuhakikishe fedha zinapatikana kwa namna yoyote ile ili miradi isikwame," aliagiza MNEC huyo. Akithibitisha ukubwa ...

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MAONESHO YA KIMATAIFA YA NANE NANE JIJINI DODOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili na kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane kwa mwaka 2026 yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya John Malecela Jijini Dodoma. Makamu wa Rais ni mgeni rasmi katika Siku Maalum ya Ushirika na Maadhimisho ya Miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inayofanyika leo tarehe 03 Agosti 2026 katika Maonesho ya Nane Nane Dodoma.

MATUNDA YA ZIARA YA RAIS SAMIA URUSI YAANZA KUONEKANA

 ….Kampuni ya Betaren yaanza kuingiza mbegu bora aina ya Bombadier, Daha, Bazik na Krechet Na Mwandishi Wetu Ziara ya kikazi ya siku tatu aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi Juni 3 mwaka huu imeanza kulipa baada ya kampuni za kutoka nchini humo ikiwemo Betaren kuja kuwekeza kwenye mbegu za kisasa za mazao. Kampuni ya Sky Business and Investment Company Ltd imeingia ubia na kampuni hiyo yenye asili ya Urusi ya Betaren kwaajili ya kusambaza mbegu bora za kisasa, mbolea na viuatilifu kwa wakulima Tanzania. Aina ya mbegu ambazo kampuni hiyo imeanza kuingiza nchini ni pamoja na mbegu aina ya Bombadier, Daha, Bazik na Krechet ambazo ziko kwenye hatua za mwisho kupata kusajili. Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya nane nane mkoani Dodoma, Mbunge wa Kisarawe, Seleman Jafo alisema ujio wa kampuni hiyo kuwekeza nchini ni matokeo ya diplomasia ya uchumi ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyetembelea Urusi hivi karibuni. Alisema wawekezaji kuto...

MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO YABEBA MAPINDUZI YA KIDIJITALI SEKTA YA KILIMO

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imesema matumizi ya teknolojia ya kidijitali yamekuwa chachu ya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo nchini, yakirahisisha utoaji wa huduma za Serikali, kuongeza uwazi na kuwainua wakulima kupitia mifumo bunifu inayowezesha huduma kupatikana kwa haraka na kwa ufanisi. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Meneja wa Mawasiliano wa e-GA, Subira Kaswaga, alisema mamlaka hiyo imeendelea kuwekeza katika ujenzi na uboreshaji wa mifumo ya kidijitali inayounganisha taasisi za Serikali na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, e-GA imeunda mfumo wa e-Kilimo, unaowezesha ukusanyaji wa taarifa za wakulima, usimamizi wa taasisi zilizo chini ya wizara pamoja na utoaji wa vibali mbalimbali vinavyohusiana na shughuli za kilimo. "Tunatumia teknolojia kuhakikisha huduma za Serikali zinakuwa rahisi, za haraka na zenye uwazi zaidi, huku sekta ya kilimo ikinufaika kwa kuongeza ti...

NEEMA ZAO LA MKONGE: SERIKALI YASHUSHA MASHINE 10 MPYA, USHIRIKA KUKOPA BILIONI 11 KUSIMIKA MITAMBO

Na Mashaka Mhando, DODOMA KATIKA hatua ya kukuza zao la mkonge nchini na kuongeza ubora wake kwenye masoko ya ndani na nje, Serikali imetangaza mpango wa kununua mashine 10 mpya za kuchakata zao hilo (Dikotiketa/Korona) kwa ajili ya wakulima wadogo.  Sambamba na hilo, Vyama vya Ushirika (AMCOS) vitano wilayani Korogwe, vinatarajiwa kuwekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 11.5 kupitia mikopo ya benki kwa ajili ya kusimika mitambo mipya ya kisasa ya kuchakata mkonge. Lengo la hatua hizo ni kuhakikisha zao hilo linaendelezwa kwa tija, na kuwasaidia wananchi walioamua kulifanya mkonge kuwa zao lao kuu la biashara kupata fursa ya kuvuna na kusindika katika viwango vya ubora wa kimataifa. Mkakati huo umetangazwa Agosti 2, 2026, na Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Mkonge kutoka Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Bw. Simon Kibasa, wakati akizungumza kwenye Maonesho ya 33 ya Kitaifa ya Kilimo (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, jijini Dodoma. Usambazaji wa Mashine ...