Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TARURA MKOA WA LINDI YAPOKEA TUZO YA UKIDHI WA SHERIA YA MANUNUZI WA UMMA

📌Tarura Yapokea Tuzo Tatu za PPRA Arusha  TARURA Mkoa wa Lindi imepata tuzo ya Ukidhi wa Sheria ya Ununuzi wa Umma kufuatia ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Tuzo hiyo imetolewa katika Kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma, ikiwa ni kutambua uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma pamoja na kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za umma. TARURA Lindi inaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yake unazingatia misingi ya utawala bora na matumizi yenye tija ya fedha za umma.

MAWAKILI WA SERIKALI WANOLEWA KUHUSU SHERIA YA FEDHA

 Mwandishi Mkuu wa Sheria, Bw. Onorius Njole amefungua mafunzo maalum kwa Mawakili wa Serikali nchini, yanayohusu Sheria ya Fedha (Finance Act). Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 30 Julai, 2026 Jijini Dodoma, ambapo Mawakili wa Serikali kutoka taasisi mbalimbali nchini wameshiriki kwa wingi katika mafunzo hayo kwa njia ya mtandao.  Mafunzo ya Sheria ya Fedha kwa Mawakili wa Serikali, yameratibiwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria, na kuendeshwa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na Wizara ya Fedha. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwandishi Mkuu wa Sheria, ameeleza kuwa Sheria ya Fedha ni mhimili mkuu wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali, hivyo Mawakili wa Serikali wana mchango mkubwa katika kuchambua, kuandika, na kuhakikisha vifungu vyake vinakidhi mahitaji ya kisheria na kiuchumi.  *“Mafunzo haya yanalenga katika kuwapitisha Mawakili wa Serikali ili muweze kufahamu nafasi yenu ...

DC KYOBYA MGENI RASMI TUKIO LA KIHISTORIA "HIKE FOR A GIRL CHILD" UDZUNGWA

 KILOMBERO  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Msomi Dkt. Dunstan Kyobya anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye tukio la kihistoria la Matembezi ya Vilimani ili kupaza Sauti kwa Ajili ya Mtoto wa Kike, _"Hike for A Girl Child"_. Tukio hilo lenye lengo la kuvunja ukimya na unyanyapaa masuala ya Hedhi Salama kwa Watoto wa Kike, litafanyika tarehe 2 Agosti 2026, katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa, Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro. Kwa mujibu wa Waratibu wa kampeni hiyo kutoka The Brighter Binti Foundation, Dkt. Kyobya anatarajiwa kuzindua daraja la Utalii katika njia ya Sonjo Route tayari kwa matembezi ya vilimani. "Agosti 2, saa 1:00 Asubuhi, Mkuu wa Wilaya Dkt. Kyobya atazindua rasmi daraja la Utalii, kisha kufanya 'Hike' njia ya maporomoko ya maji ya Sanje ambapo washiriki wote tutajumuika," wamesema waratibu hao. Mchana, matukio mengine yatafanyika Shule ya Sekondari Sanje ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo: Mawasilisho mafupi ju...

SERIKALI NA WAWEKEZAJI & WATOA HUDUMA MIGODINI WAJADILI CHANGAMOTO NA MAFANIKIO KWENYE SEKTA YA MADINI*

▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira rafiki ya uwekezaji ▪️ Wadau wapongeza hatua za serikali za kutatua changamoto ▪️Waziri Mavunde awataka Watanzania kuanza ujenzi wa viwanda vya bidhaa za migodini ▪️ Kampuni ya MANTRA yanuia kuiweka Tanzania kwenye kumi bora ya wazalishaji wa Uranium Duniani Dar es salaam Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya madini kupitia majukwaa ya majadiliano kwa lengo la kujenga sekta yenye ushindani, inayovutia uwekezaji na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Mhe. Mavunde ameyasema hayo katika kikao cha Mining Breakfast Briefing (*MBB*), kilichoandaliwa kwa ushirikiano wa Chemba ya Migodi Tanzania(TCM) na Wizara ya Madini, ambapo ametoa wito kwa wadau kuendelea kutumia majukwaa hayo kujadili fursa na changamoto zinazohusu sekta ya madini. Amewashukuru viongozi na wanachama wa Chemba ya Migodi Tanzania kwa kuendelea kutoa nafasi ya Serikali na wadau kukutana na kujadiliana kuhus...

RAIS SAMIA AIPA TADB NGUVU,MTAJI WAPAA HADI BILLIONI 452.16

Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha sekta ya kilimo zimeendelea kuzaa matunda baada ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuongeza mtaji wake kutoka Shilingi bilioni 60 hadi kufikia Shilingi bilioni 452.16, hatua inayoongeza uwezo wa benki hiyo kufadhili kilimo, mifugo na uvuvi kwa kiwango kikubwa zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 30, 2026, katika ukumbi wa Idara ya Habari  MAELEZO jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania TADB, Frank Nyabundege, amesema mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali pamoja na ushirikiano na taasisi mbalimbali za maendeleo. Amesema kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaji wa TADB ulikuwa Shilingi bilioni 60 pekee, lakini sasa umefikia Shilingi bilioni 452.16, jambo linaloifanya benki hiyo kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi nchini. "Kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaji wa ...

JAB YAANZA NA BONGO FM MAFUNZO RASMI YA WAANDISHI WA HABARI

 Mwandishi Wetu, Dar es Salaam, Julai 29, 2026 Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeanza rasmi kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini, yakilenga kuimarisha weledi, maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari wa Bongo FM jijini Dar es Salaam, redio dada ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya JAB, Tido Mhando, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kuelewa na kutekeleza matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229, kwa kuzingatia weledi, maadili na uwajibikaji. “Mafunzo haya ni utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari. Leo tumeanza rasmi na waandishi wa habari wa Bongo FM, tutaendelea kwa vyombo vingine pia kwa sababu, kutakuwa na mafunzo ya muda mfupi na ya muda mrefu. Hivyo, mafunzo haya yawe fursa ya kujenga uwezo na kuweka msingi imara wa kukuza na kulind...