Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ameshusha mbao zaidi ya 35000 kwaajili ya utengenezaji wa madawati,viti na meza kwa shule za msingi na sekondari. Mbao hizo zimeteremshwa leo februari 20/2025 kwenye eneo la utengenezaji shule ya msingi Mukendo na kupokelewa na diwani wa Kata ya Nyakato Joseph Tikina Kisunda. Akizungumza mara baada ya kupokea mbao hizo diwani huyo amesema mbunge Mathayo amedhamiria kuondoa kero ya madawati,viti na meza kwa shule za msingi na sekondari manispaa ya Musoma. Amesema mbunge ameaxgiza mbao nyingi ambazo zikitengenezwa vifaa hivyo itawafanya wanafunzi kukaa kwa nafasi na kupata elimu bora. Kitina amesema mbunge Mathayo anastahili kupongezwa kwa kuthamini elimu ya mtoto wa jimbo la Musoma mjini. Diwani huyo amesema anaamini baada ya mafundi kupokea watatengeneza na kukamilika kwa wakati. " Tunamshukuru sana mbunge Vedastus Mathayo kwa kuagiza na kuleta mbao kwaajili ya utengenezaji wa madawati,viti ...
Marato tv - Sauti ya Jamii