Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha sekta ya kilimo zimeendelea kuzaa matunda baada ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuongeza mtaji wake kutoka Shilingi bilioni 60 hadi kufikia Shilingi bilioni 452.16, hatua inayoongeza uwezo wa benki hiyo kufadhili kilimo, mifugo na uvuvi kwa kiwango kikubwa zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 30, 2026, katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania TADB, Frank Nyabundege, amesema mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali pamoja na ushirikiano na taasisi mbalimbali za maendeleo. Amesema kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaji wa TADB ulikuwa Shilingi bilioni 60 pekee, lakini sasa umefikia Shilingi bilioni 452.16, jambo linaloifanya benki hiyo kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi nchini. "Kabla ya Serikali ya Awamu ya Sita, mtaji wa ...
Marato tv - Sauti ya Jamii