Katika hatua za kukuza Sekta ya Usafirishaji na Utatuzi wa changamoto katika jamii, Wizara ya Uchukuzi imeipongeza kampuni ya UTEGI Limited kwa kufanikisha uwekezaji katika nyanja ya usafirishaji kupitia Kampuni ya Plug & Ride Tanzania iliunganisha maitaifa ya Tanzania na India.
Akizungumza mapema hii leo, Naibu Waziri, Wizara ya Uchukuzi Mhe. David M. Kihenzile kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi , Profesa Makame Mbarawa, wakati aliposhiriki katika hafla ya Uzinduzi wa kampuni ya Plug & Ride Tanzania, inayojihusisha na usambazaji na uundaji wa vyombo vya usafiri vinavyotajwa kwenda kupunguza hadha ya kubebea wagonjwa na watoto wa shule katika hospitali na shule mbalimbali nchini.
Aidha, Amepongeza ujio wa uwekezaji huo ambapo amesema utaenda kuchangia uchumi wa Taifa, ikiwa ni pamoja na kuendeleza sera ya utunzaji mazingira kwa matumizi ya umeme pamoja na kuongeza idadi ya ajira kwa vijana wa kitanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Aristides Mbwasi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema kuwa sekta ya viwanda inalenga kuongeza kiasi cha ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 8 hadi kufikia aslimia 15 katika utekelezaji wa dira ambapo pia amesema Tanzania kwasasa inaongoza katika Afrika Mashariki kwa kuwa na vyombo vinavyotumia umeme zaidi ya elfu kumi.
Nae, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji (Uwekezaji), Dkt. Fred Msemwa, anesema kuwa uwekezaji huo unaozinduliwa unakwenda kuleta utatuza wa matatizo ya watanzania katika sekta ya usafirishaji kwa jamii zote za kitanzania kwa ujumla.
Kwa Upande wake, Bwa. Otieno Olunga Igogo, Mmiriki na Mwanzilishi wa kampuni ya Utegi Technical Enterprises (T) Limited na Makamu Mwenyekiti wa kampuni ya Plug & Ride Tanzania amesema kutokana na changamoto za jamii za kitanzania ameamua kuja na ubunifu wa 'Ambulance' ya matairi matatu ili kuweza kusaidia kusafirisha wagonjwa ikiwa pamoja ujio wa bajaj za kubebea wanafunzi wa shule za awali hii ikiwa ni kutambua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa kuelekea mashuleni.
Hata hivyo Igogo ameeleza kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali kampuni yake imelenga kuja na vyombo vya umeme ili kupunguza ghalama za maisha ikiwa sambamba na kuongeza ajira endelevu pamoja na kuongeza thamani katika kazi wanazozifanya maafisa usafirishaji maqrufu kama bodaboda.
Igogo ameongeza kuwa kufuatia uwepo wa uwekezaji huo unalenga kwenda kutokomeza changamoto za upatikanaji wa mafuta dunia, huku akisema upatikanaji wa vyombo hivyo ni rafiki na ghalama nafuu zaidi.
Aidha, Igogo ameipongeza Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji yaliyowezesha kuanzishwa kwa mradi huo wa ubia kati ya Tanzania na India.
Ujio wa kampuni ya Plug & Ride Tanzania, unaongeza kasi ya matumizi ya teknolojia za kisasa zinazolenga usafiri wenye ufanisi na rafiki kwa mazingira ya kitanzania na ni hatua inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika matumizi ya magari na pikipiki za umeme nchini.
Suluhisho la usafiri wa kisasa kupitia uwekezaji wa Plug & Ride Tanzania unatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia uundaji wa ajira, uhamishaji wa teknolojia na kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya viwanda na nishati safi nchini.
Huku kampuni hiyo pia inaonesha kuendelea kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania, huku ukitoa fursa kwa wananchi na taasisi mbalimbali kunufaika na teknolojia mpya za usafiri hatua hiyo inaendana na jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na maendeleo endelevu.





Comments
Post a Comment