Vyama Vya siasa vyaagizwa kufuata Sheria ya uchaguzi

GEORGE MARATO TV
0




Na MASHAKA MHANDO, Tanga

VYAMA vya siasa mkoani Tanga, vimetakiwa kufuata kanunu, taratibu na Sheria ya uchaguzi kuchagua wanaendesha kampeni zenye na upendo ili uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu ufanyike kwa amani.


Akizungumza katika semina ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa Jiji la Tanga Leo Septemba 11, Ofisa Mwandamizi wa ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Edna Assey alisema vyama vinapaswa kufuata Sheria na waepuke kampeni zenye viashiria vya uvunjigu wa amani nchini.

Alisema kuwa wajibu wa vyama vya siasa ni uchaguzi na kushinda baada ya wananchi kuridhika na sera za vyama vyao wanazofanya mikutano ya kampeni.

Ofisa huyo alisema viongozi hao wafuate taratibu za uchaguzi ambazo ni mbili za Vyama vya siasa Sheria namba 257 na Sheria namba 278 za gharama za uchaguzi.

"Najua viongozi mnajua Sheria hizi, mtazifuata lakini mtafanya kampeni za kistaarabu ambazo zitasababisha uchaguzi wetu unafanyika kwa Amani na haki," alisema.

Pia aliwataka kuhakikisha kuwa endapo kuna changamoto zinazokiuka maadili au mwingiliano wa makusudi baina chama na chama wasisite kutoa malalamiko yao ili yafikishwe Kamati ya maadili.

"Kama katika eneo lako kuna changamoto ya nwingiliano wowote mtawasilisha malalamiko yenu na hakikisha jambo hilo ni la kweli mkijua kwamba hutoa taarifa ya uongo ni kosa kisheria," alisema.

Semina hiyo imeshirikisha makatibu na wenyeviti wa vyama vya siasa kutoka wilaya za Tanga, Pangani, Muheza na Mkinga.

Awali akifungua semina hiyo uchaguzi wa uchaguzi Jimbo la Tanga, Bahati Kahindi alisema jumla ya vyama vya siasa 12 vimesimamisha katika nafasi ya Ubunge na udiwani isipokuwa kata moja ya Kiomoni kati ya kata 27 zilizopo Jijini Tanga.

Alisema kuwa hadi Sasa hakuna changamoto iliyojitokeza katika Jiji hilo na kwamba amewaeleza viongozi hao ratiba za vyama vyao kuruhusu kubadilika kulingana na taratibu au mwongozo mwingine.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top