Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SERIKALI YAIMARISHA MALEZI, ULINZI NA USTAWI WA WATOTO NCHINI


 WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali imeendelea kuimarisha malezi, ulinzi na ustawi wa watoto nchini kupitia programu mbalimbali zinazolenga kujenga kizazi chenye maadili, afya bora na uwezo wa kuchangia maendeleo ya Taifa.

Dkt. Gwajima alisema hayo leo Juni 1, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Amesema watoto ni rasilimali muhimu na mtaji wa Taifa, hivyo wanapaswa kulelewa katika mazingira salama, yenye upendo na maadili mema ili kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kwa mujibu wa waziri Gwajima, Amesema Serikali inaendelea kutekeleza Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (2021/22–2025/26), inayolenga kuongeza kiwango cha ukuaji timilifu wa watoto wenye umri chini ya miaka minane kutoka asilimia 47 hadi asilimia 90 ifikapo mwaka 2050.

Amesema katika kuimarisha malezi ya watoto, Wizara imeanzisha mifumo ya kisasa ya kukusanya na kufuatilia takwimu za malezi na makuzi ya watoto, huku maafisa 227 kutoka ngazi mbalimbali wakipatiwa mafunzo ya usimamizi wa mifumo hiyo.

Dkt. Gwajima Amesema Serikali imeongeza juhudi za kulinda watoto dhidi ya ukatili mtandaoni kufuatia ongezeko la matumizi ya teknolojia, ambapo takwimu zinaonesha asilimia 67 ya watoto wenye umri wa miaka 12 hadi 17 hutumia simu janja.

Ameeleza kuwa wawezeshaji 516 walipatiwa mafunzo ya usalama wa watoto mtandaoni na kufanikiwa kuwafikia wanafunzi zaidi ya milioni 1.8, walimu 679 pamoja na watumishi wasio walimu 232 katika mikoa yote 26 nchini.

Aidha, Amesema Serikali imeanzisha Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni na ipo katika hatua za majadiliano ya kuanzisha matumizi ya Laini Maalumu ya Simu kwa Mtoto (Child SimCard) kwa lengo la kuongeza usalama wa watoto katika matumizi ya teknolojia na mawasiliano.

Katika kuimarisha ulinzi wa mtoto shuleni, walimu 4,388 wamepatiwa mafunzo ya kusimamia afua za ulinzi na usalama wa mtoto huku madawati 3,204 mapya ya ulinzi wa mtoto yakianzishwa na kufanya jumla kufikia madawati 11,156 nchini.

Serikali pia imeendelea kuwashirikisha watoto katika maamuzi yanayowahusu kupitia Mabaraza ya Watoto, ambapo mabaraza 223 mapya yameanzishwa na kufanya jumla kufikia 8,427 kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa.

Katika vita dhidi ya ukeketaji, Dkt. Gwajima Amesema Serikali imezindua Mkakati wa Taifa wa Kisekta wa Kutokomeza Ukeketaji wa mwaka 2025/26 hadi 2029/30 unaolenga kupunguza kiwango cha ukeketaji kutoka asilimia nane hadi asilimia nne ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wa watoto walio katika mazingira hatarishi, Amesema zaidi ya watoto 284,000 wametambuliwa na kupatiwa huduma mbalimbali za kiustawi ikiwemo elimu, afya, mafunzo ya ufundi stadi na kuunganishwa na familia zao.

Aidha, watoto 6,182 waliokuwa wanaishi na kufanya kazi mtaani wameokolewa kupitia kampeni maalumu ya kitaifa, huku Serikali ikianzisha madawati 14 ya huduma za ustawi wa jamii katika vituo vikuu vya usafiri nchini yaliyosaidia kuokoa watoto 3,366 na kuwaunganisha na familia zao.

Katika kulinda haki za watoto kupitia mfumo wa sheria, mashauri 1,367 yalisikilizwa katika Mahakama za Watoto kati ya Julai 2025 na Aprili 2026, huku watoto 154 waliokinzana na sheria wakipatiwa huduma za marekebisho ya tabia na stadi za maisha katika vituo maalumu.

Waziri Gwajima Amesema Serikali imeendelea pia kuimarisha huduma za malezi ya awali kwa kusajili vituo 922 vya kulelea watoto mchana, na kufanya jumla ya vituo hivyo kufikia 4,916 vinavyohudumia watoto zaidi ya 565,000 nchini.

Pamoja na mafanikio hayo,Amesema changamoto ya ukatili dhidi ya watoto bado ipo, ingawa takwimu zinaonesha idadi ya watoto walioripotiwa kufanyiwa ukatili wa kingono imepungua kutoka 10,937 mwaka 2024 hadi 9,902 mwaka 2025.

Dkt. Gwajima Amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya ukatili wa watoto si jukumu la Serikali pekee bali ni wajibu wa jamii nzima, ikiwemo wazazi, walezi, viongozi wa dini, walimu na wananchi kwa ujumla kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama, yenye maadili na heshima kwa utu wa binadamu.

zaidi ya wazazi na walezi 469,634 wamepatiwa elimu ya malezi chanya kupitia majukwaa mbalimbali nchini, huku vikundi 4,526 vya malezi na matunzo ya watoto vikianzishwa chini ya kaulimbiu ya "Familia Bora, Taifa Imara."

Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...