Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Wananchi mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza kuchukua vitambulisho vyao vya uraia na walio fikisha umri wa miaka kumi na nane (18) kujiandikasha, na sio kujiandikasha Kwa mahitaji maalum.
Wito huo umetolewa na Afisa usajili mamlaka ya vitambulisho mkoa wa Tanga Ayoub Mwenda akiwa na lengo la kupunguza msongamano kwana wananchi wamekuwa wakisubiri fursa zitikee ndio waanze kutafuta nyaraka muhimu ikiwemo vitambulisho vya uraia jambo ambalo sio sawa kwani wao hutumia mtandao na Kuna wakati mtandao huo hushindwa kufanya kazi Kwa ufanisi na mwisho wa siku lawama kutupiwa kwao.
Pamoja na hayo pia amewataka wale ambao walipatiwa vitambulisho vyenye kasoro kama kufutika vyenyewe wavirudishe mara mojakatika ofisi za NIDA kwani serikali ipo tayari kuvifanyia marekebisho na kuwapatia vitambulisho vyenye ubora bila gharama yoyote.
Mwenda ameongeza kuwa kwasasa mambo yamerahisishwa zaidi kwani mtu anauwezo wa kujisali mwenyewe mtandaoni kupitia tovuti yao bila kufika ofisini kwakuwa maelekezo yote yapo wazi na hii ikiwa na lingo la kupunguza usumbufu Kwa wananchi.
"Niwaombe wananchi kujiandikasha mapema mtu anapofikisha miaka 18 na sio kusubiri mpaka kihitajike kwani Kwa kufanya hivyo itapunguza msongamano na kuokoa muda kwa wahitaji,sisi tunatumia mfumo kunawakati mfumo huelemewa na kushindwa kufanya kazi Kwa ufanisi na mwisho wa siku lawama huja kwetu maofisa kumbe inaweza kuepukika Kwa kufanya mambo mapema", Mwenda.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Fatma Ally amesema kuwa kwasasa mambo sio magumu na wala hakuna usumbufu ukifika katika ofisi za NIDA na vielelezo vyako vyote kama kitambulosho cha mpiga kura,kadi ya kliniki,leseni ya uderva na taarifa za wazazi zikiwa sahihi.


Comments
Post a Comment