Mwenyekiti wa Taasisi ya Mkono wa huruma Tanzania (MWAHUTA), Araphaty Japhary Mayala amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuchinja takribani ng’ombe 700 mwaka huu kwa ajili ya kugawa nyama kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza huduma za kijamii na kusaidia wananchi wasiojiweza.
Matendo hayo ya huruma ni kutokana na mafundisho ya dini ya kiislamu kama anavyosema Mwenyezi Mungu katika QUR'AN tukufu inapofika sikukuu ya Eid ul-Adha ni vema kuchinja Mnyama ili Kutoa sadaka Kwa jamii inayokuzunguk
Akizungumza jijini Dodoma, wakati akitekeleza ibada ya kuchinja Mayala amessema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau, viongozi wa serikali, viongozi wa mitaa na wananchi walioshiriki kufanikisha zoezi hilo muhimu.
Mayala pia Ametoa shukrani za dhati kwa viongozi wote waliowaunga mkono, hususan Mkuu wa Wilaya ambaye alisema amekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa ulinzi na huduma za madaktari kwa ajili ya ukaguzi wa nyama kabla ya kusambazwa kwa wananchi.
“Tunawashukuru sana wadau wetu wote, viongozi wa serikali, viongozi wa mitaa na wananchi waliotuunga mkono. Ushirikiano wao umewezesha kufanikisha zoezi hili kwa amani na utulivu mkubwa,” amesema Mayala.
Amesema lengo la taasisi hiyo ni kuhakikisha msaada huo unawafikia watu wanaouhitaji zaidi, hivyo aliwataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kufuata utaratibu uliowekwa wakati wa ugawaji wa nyama.
Mayala Amesema kutokana na idadi kubwa ya watu wanaohitaji huduma hiyo, ni muhimu kila mmoja kuheshimu utaratibu ili kutoa nafasi kwa wale walio katika mazingira magumu zaidi kunufaika na msaada huo.
“Tunapenda kuona kila anayestahili anapata sehemu yake. Ndiyo maana tunaomba ushirikiano, uvumilivu na kuheshimu utaratibu uliowekwa ili haki itendeke kwa wote,” amesisitiza.
Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kuwa MWAHUTA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutekeleza shughuli za kijamii zenye lengo la kusaidia makundi yenye uhitaji na kuimarisha mshikamano ndani ya jamii.
Sambamba na hayo ametoa shukrani kwa wananchi wote walionufaika na zoezi hilo pamoja na viongozi waliojitokeza kushiriki na kulisapoti, akisema hatua hiyo inaonesha umuhimu wa mshikamano katika kuwasaidia wenye uhitaji na kujenga jamii yenye upendo na kujali.





Comments
Post a Comment