MAMCU yauza Tani 8295 za mbaazi kwa bei ya juu 850 na Bei ya chini 81 msimu wa kilimo 2025.......

GEORGE MARATO TV
0

Mnada rasmi wa zao la mbaazi kwa msimu wa mwaka 2025/2026 umezinduliwa katika kijiji cha Lukuledi, Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. 

Uzinduzi huo umefanyika kwa usimamizi wa Afisa Biashara na Masoko, Bi Neema Mmavele, ambaye alieleza kuwa jumla ya tani 8,295.197 za mbaazi zinatarajiwa kuuzwa sokoni msimu huu. 

Bi Mmavele alisema kuwa ni matarajio yao kuona wanunuzi wa zao hilo wakijitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wakulima wanapata soko la uhakika. 

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika (MAMCU), Bakari Ado, alifafanua kuwa mzigo wa mbaazi uliofikishwa mnadani ni tani 8,295, huku baadhi ya shehena (loti) tatu — yaani loti 50, 52 na 58 — zimeshindwa kuingia mnadani.

 Ado alibainisha kuwa kulikuwa na jumla ya loti 61 na zote, isipokuwa hizo tatu, hazikufanikiwar kupata wanunuzi.

 Aliongeza kuwa bei ya juu katika mnada huo ilikuwa shilingi 850 kwa kilo, huku bei ya chini ikiwa shilingi 810.

Katika kuhakikisha uadilifu wa vipimo wakati wa uuzaji wa mazao, Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Mtwara, Saidi Huruma Seif, aliwataka wakulima na wanunuzi kuhakikisha mizani yote inayoenda kupimia mazao imehakikiwa rasmi. 

Alisema mizani halali itawekwa stika pamoja na muhuri maalum (seal), na kusisitiza kuwa kama vipengele hivyo havipo, wakulima wasikubali kuuza mazao yao kwa kutumia mizani hiyo. 

Hata hivyo, wakulima wa mbaazi waliotoa maoni yao kupitia mwakilishi wao, Issa Issa, walieleza masikitiko yao juu ya bei mpya ya zao hilo. 

Issa alisema kuwa bei ya mwaka huu ya kati ya shilingi 810 hadi 850 ni ndogo mno ikilinganishwa na mwaka uliopita (2024), ambapo waliuza mbaazi kwa bei ya juu kati ya shilingi 1,800 hadi 2,000 kwa kilo. 

Alisema kuwa hali hiyo imewakatisha tamaa na kuvuruga matarajio yao ya kupata faida kutokana na kilimo cha mbaazi. 

Wakulima sasa wana matumaini kuwa wadau wa sekta ya kilimo wataingilia kati ili kuhakikisha bei za mazao hususani mbaazi zinakuwa na tija kwa mkulima. Wanasisitiza haja ya kuwepo kwa mikakati ya kudumu ya kuimarisha soko na kudhibiti uporomokaji wa bei, ili kulinda maslahi ya mkulima wa kawaida.










Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top