Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Kambarage Masato Wasira, leo Julai 13, 2026, ameungana na viongozi mbalimbali wa Serikali kushiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na umehudhuriwa na viongozi wa Serikali, mawakili wa Serikali kutoka taasisi mbalimbali, pamoja na wadau wa sekta ya sheria na haki.
Ushiriki wa Mhe. Kambarage Wasira katika mkutano huo unaonyesha umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za Serikali na wadau wa sekta ya sheria katika kukuza utawala bora, kuimarisha misingi ya haki na kuendeleza maendeleo ya taifa kupitia mifumo imara ya kisheria.
Mkutano Mkuu wa TPBA hufanyika kila mwaka ukiwa jukwaa la kujadili masuala ya taaluma ya sheria, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha utendaji wa mawakili wa Serikali katika kuhudumia wananchi na kulinda maslahi ya Taifa.




Comments
Post a Comment