Aidha Mhe Mbunge *Massaburi* alipata wasaa wa kuongea na wananchi waliohudhuria katika hafla iyo huku akiwashukuru Kwa mapenzi yao makubwa licha ya mvua kubwa lakini walijotokeza Kwa wingi katika hafla iyo.
Pia Mhe Mbunge *Massaburi* alimpongeza mkuu wa shule Ndugu. Kuwa mfano wa kuigwa katika Jimbo la kivule Kwakua amekua ni Mtu wa kutatua changamoto na sio kulalamika. Aidha aliwashukuru wadau mbalimbali wakiwemo *Shivuta* na wengine Kwa uchangiaji wao hasa kununua vifaa vya *TEHAMA* ambavyo amevikabidhi leo.
Mwisho Mhe Mbunge *Massaburi* aliwapongeza wananchi Kwa juhudi zao za kuanza kuchangia ukuta wa shule na kwakua wamekua wazalendo aliomba uongozi wa shule ye kama Kiongozi wao atatoa kiasi cha *shilingi Milioni Tisa na laki nne ( 9,400,000)* yeye pamoja na marafiki zake. Pia Mhe Mbunge *Massaburi* alisisitiza zoezi la kujenga ukuta lianze mara Moja, Katika ziara iyo Mhe Mbunge Massaburi aliongozana na Diwani kata ya Majohe *JULIUS WARIOBA GEKULA* pamoja na viongozi wa *Chama cha mapinduzi.*



















Comments
Post a Comment