Na Jovina Massano- Musoma.
Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Ukombozi wa Umma CHAUMA Jimbo la Musoma mjini Angela Derick Lima amesema upandishaji hadhi chuo Cha Maendeleo ya Jamii kilichopo Kata ya Buhare Jimbo la Musoma mjini kutawezesha Maendeleo na ukuaji wa uchumi katika Kata.
Ameyasema hayo Septemba 25,2025 wakati akinadi Sera za chama hicho katika kata ya Buhare Jimbo la Musoma mjini mkoani Mara.
Anjela amesema endapo serikali ingepandisha hadhi Chuo Cha Maendeleo ya Jamii kilichopo Kata ya Buhare ingewezesha ukuaji wa uchumi katika eneo hilo na kuongeza Maendeleo ya wananchi.
Amesema upandishaji hadhi utawezesha ongezeko la watu ambapo wakazi wa eneo hilo watafanya shughuli na kutoa huduma Mbalimbali na kuwezesha upatikanaji wa ajira na kujiajili na kujiletea Maendeleo.
Kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukoaefu wa soko la pamoja, miundombinu mibovu ya barabara na ukosefu wa wodi ya akina mama.
"Kwa kushirikiana na serikali nitakwenda kusukuma huduma za kijamii ili kuwawezesha ustawi wa uchumi katika Kata hii ya Buhare", amesema Angela.
Lakini pia ameahidi kuweka mfuko kwa ajili ya wanafunzi wenye Mazingira magumu ili kuwawezesha kufanikisha safari yao kielimu kuleta usawa.
Sanjari na hayo ameongelea umuhimu wa kuwajengea uwezo makundi yanayokwenda kuchukua mikopo ya asilimia 10 kwa kupata elimu ya nidhamu ya fedha na kuelekeza kwenye matumizi sahihi waweze kurejesha bila changamoto.