Mavunde Aendelea na Kampeni za Mtaani Kwa Mtaani Kata ya Ihumwa

GEORGE MARATO TV
0


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Anthony Mavunde, ameendelea na awamu ya kwanza ya kampeni zake kwa kuzungukia mitaa mbalimbali ya Kata ya Ihumwa.

Katika ziara hiyo,Ndugu  Mavunde alikutana na wananchi wa Mitaa ya Chang’ombe, Chilwana, Ilolo na Ihumwa ambapo alisikiliza changamoto zao na kuwasilisha sera za chama chake.

Akizungumza na wananchi leo Septemba 25,2025, ndugu Mavunde amesema: “Nimekuja kusikiliza maoni na changamoto zenu ili tuzitatue kwa pamoja. Kura zenu kwangu na kwa wagombea wa CCM zitasaidia kuendeleza kasi ya maendeleo katika Jimbo la Mtumba, " amesema

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kumpa kura za ushindi pamoja na kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Mgombea Udiwani wa Kata ya Ihumwa, Edward Magawa.

“Naomba tushirikiane kumpa kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa urais, diwani wenu Edward Magawa, na mimi kwa ubunge, ili kwa pamoja tuendelee kuwaletea maendeleo yenye tija,” amesema Mavunde.










Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top