Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amewata wananchi mkoani humo kuachana na imani potofu za kutokupeleka wagonjwa hospitali na kuishia kwa waganga wa kienyeji.
Amesema zama hizo zimepitwa na wakati kwani kwa sasa teknolojia imekuwa na huduma za afya zimeboreshwa nchini kwa kuwa na vifaa tiba vya kisasa.
Mtaka Ameyasema hayo mkoani Njombe alipokuwa akizindua kambi ya siku 21 ambayo itatoa huduma ya vipimo mbalimbali bure kwa kila mwananchi atakayefika katika kambi hiyo
“Unakuta mtu amepata ugonjwa wa kiharusi au sukari badala ya kwenda kwenye vipimo anakimbilia kwa mganga wa kienyeji ambako hawezi kupata huduma inayotakiwa na ugonjwa unaendelea kuwa sugu mwisho wa siku anakufa” amesema Mtaka







