Na Mwanamkuu Mwandoro,Tanga .
CHAMA cha Mafundi Tanga (CMT)kufuatia juhudi zake za kupiga vita vilainishi visivyo faa(vilainishi feki) kimefanikiwa kuungwa mkono na Mbunge wa jimbo la Tanga Kassim Mbaraka na kuahidi kuwa mlezi wao na kiwasaidia.
Mbaraka amefikia maamuzi hayo ikiwa lengo ni kuunga mkono kauli ya waziri wa viwanda na biashara inayotaka kutokomeza bidhaa feki hasa za vilainishi visivyo faa (oil feki).
Nae Mkurugenzi wa S.S.M.C Limited ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha Mafundi TANGA(CMT) Bw. Said Selemani Mohamed maarufu(Said Kijiko) amesema wao Kwa umoja wao wamempokea Kwa faraha mlezi huyo.
Aidha Kijiko ameongeza kuwa kufuatia uwepo wa kiwanda cha MOGAS Tanga ni vema wananchi wakatumia bidhaa kutoka huko ili kulinda mashine zao kudumu Kwa muda mrefu na kuepuka gharama zinazo epukika.
Sambamba na hayo CMT wamejipanga kutoa elimi Kwa wananchi ili kuwaongezea uelewa wa namna ya kugundua vilainishi visivyo faa na vinavyofaa.



