Taulo za kike kuongeza ufaulu Kwa Wanafunzi Misungwi

GEORGE MARATO TV
0


Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi Bw.Christopher Legonda ameongoza Zoezi La Ugawaji wa Taulo za Kike zilizo nunuliwa na Halmashauri ya Wilaya Kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri kwa Lengo la Kuongeza Ufaulu kwa Wanafunzi mapema leo tarehe 11/05/2026 katika Viwanja vya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.

Amesisitiza kuwa Serikali Itaendelea Kuboresha Miundo Mbinu Mbalimbali Mashuleni Ikiwemo Vyumba vya Kujifunzia Ili Vikalete Tija Kwenye Ufaulu wa Wanafunzi pamoja na Kuendelea Kushilikiana na Wadau Mbalimbali wa Maendeleo Wilayani Misungwi.


Kwa Upande wake Afisa Elimu Makundi Maalumu Wilaya ya Misungwi Ndugu.Felician Malongo amewaomba Wadau Mbalimbali Kujitokeza Kuunga Mkono Jitihada Mbalimbali za Serikali Kwenye Elimu ikiwemo Hedhi Salama na Mazingira rafiki.

Naye Mwanafunzi wa Misungwi Sekondari Ms Sara Cretus amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan Kwa Jitihada Mbalimbali anazochukua Kwenye Sekta ya Elimu Ikiwemo kuboresha  Miundo Mbinu ya Kusomea,Kujifunzia na Malazi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top