Rais Samia Amesema Tutailinda Ngorongoro kwa Ajili ya Kizazi cha Sasa na Kijacho

GEORGE MARATO TV
0


 DODOMA.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro Pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Taarifa za Tume hizo leo March 12,2026 Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma ambapo amesema kuwa Ngorongoro ni maliasili adhimu inayopaswa kulindwa Kwa manufaa ya kizazi Cha Sasa na kijacho, Kwa umuhimu wake wa kipkekee katika uhifadhi wa bioanuai,utalii,historia ya mwanzo ya mwanadamu pamoja na Utamaduni wa jamii za wakazi wa asili wa eneo hilo.





Kadhalika, Rais Samia ameongeza kuwa Serikali inawajibu wa kulinda mfumo wa ikolojia unaounganisha Hifadhi ya Ngorongoro, Maeneo ya loliondo na ziwa natron ambapo amefafanua kuwa zoezi la uhamaji wa hiari lilianzishwa Kwa nia kulinda mfumo huo wa ndani ya eneo la Hifadhi wenye manufaa makubwa Kwa utalii wa nchi na urithi wa dunia.

Sambamba na hayo, Rais Samia amebainisha kuwa serikali itaendelea na utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari Kwa kirekebisha kasoro zilizobainika katika awamu ya kwanza na Kuboresha mfumo wa uratibu na utekelezaji wake,kama sehemu ya kulinda uhifadhi wa Mazingira ya asili ya eneo la Hifadhi ya ngorongoro sambamba na kuimarisha ustawi wa wananchi wakaazi wa asili wa eneo hilo.




Aidha, Rais Samia Amesema serikali imepokea mapendekezo hayo ya tume zote mbili na itayafanyia kazi Kwa lengo la kupata Suluhu ya kudumu Kwa lengo la kulinda maslahi ya wananchi, uhifadhi wa Mazingira na Ustawi wa Taifa ambapo ameielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,uratibu na Bunge kusimamia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Tume zote mbili pamoja na katibu mkuu kiongozi kuratubu utekelezaji huo. 

Akiwasilisha Ripot ya Tume ya kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika eneo la Ngorongoro,Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Katibu Mkuu Mstaafu, Mhandisi Musa Iyombe amesema kuwa ongezeko la watu, mifugo na Makazi ndani ya eneo la ngorongoro limeongeza shinikizo la Matumizi ya Ardhi na kusababisha changamoto za kimazingira ,migogoro kati ya binadamu na wanyapori pamoja na kupungua Kwa baadhi ya rasilimali za asili.

"Tume hiyo imependekeza hatua Mbalimbali za utatuzi ikiwemo mapitio ya baadhi ya Sheria, kuimarisha usimamizi wa maeneo ya Hifadhi na kuweka mikakati ya maendeleo ya Jamii nje ya eneo la Hifadhi". Amesema



Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro unalengo la kulinda maslahi ya wananchi, uhifadhi wa Mazingira na Ustawi wa Taifa.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top