Serikali imesema lishe bora mashuleni itaongeza ufaulu

GEORGE MARATO TV
0












DODOMA 

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kuwa ili kupata matokeo mazuri ya elimu ni lazima kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora shuleni ili kuwajengea wanafunzi afya bora na kupata utulivu wa akili wawapo madarasani.

Hatua hii inalenga kuboresha afya za wanafunzi na kuongeza ufaulu wao kitaaluma.


Akizungumza leo Machi 12, 2026 Jijini Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Utoaji wa chakula Shuleni Afrika kwa mwaka huu 2026,Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidhi Ameir,Amesema lishe bora kwa wanafunzi ni msingi muhimu wa kujifunza kwa ufanisi. 

Ametoa Msisitizo Kwa Wadau wa Elimu, wazazi pamoja na Jamii kwa ujumla kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula bora na maji safi wakiwa shuleni ili kuboresha afya na kuongeza ufaulu kielimu.

"Wanafunzi hutumia muda mwingi wakiwa shuleni, hivyo upatikanaji wa chakula bora, maji safi na mazingira salama ya usafi ni muhimu katika kulinda afya zao na kuongeza uwezo wa kujifunza". Amesema

“Kaulimbiu ya mwaka huu inayosema ‘Chakula Bora, Maji Safi Shuleni:Ni Wajibu wa Pamoja’ inatukumbusha kuwa jukumu la kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe bora si la Serikali pekee, bali linahitaji ushiriki wa wadau wote". Ameongeza

Kadhalika Mhe. Wanu amewasisitiza wazazi kushirikiana na shule ili kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma ya chakula shuleni kwa mujibu wa Waraka wa Elimu Na. 3 wa mwaka 2016.

Kwa upande wake Omari Singo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ambaye ni Mwakilishi wa Naibu katibu Mkuu, amesema kuwa ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI itaendelea Kushirikiana na wadau Mbalimbali nchini katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula Bora na Maji safi wakiwa Shuleni kwa lengo la Kuboresha ufaulu.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Christine Mendes amesema WFP itaendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula bora na huduma muhimu wanapokuwa shuleni ambapo amesema hakuna Mtoto anayepaswa kubaki nyuma bali kila mtoto anahaki ya kupata chakula Bora.

Maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni yalianzishwa mwaka 2016 kufuatia makubaliano ya Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, yakilenga kuhamasisha upatikanaji wa chakula na lishe bora kwa wanafunzi kupitia ushirikiano wa Serikali, mashirika ya kimataifa na jamii ambapo Kwa Mwaka huu 2026 Madhimisho hayo yanaongizwa na kauli Mbiu isemayo "Chakula Bora, Maji Safi Shuleni:Ni Wajibu wa Pamoja".

Mwisho 

              NA SALEH LUJUO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top