Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Machi 13, 2026 ametembelea Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi na kusalimiana na viongozi wa Chama hicho.
Ziara hiyo imefanyika kabla ya kuanza rasmi shughuli zake za kikazi mkoani humo, ambapo anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.



