Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini Leo Machi 18, 2025 amefanya Ziara ya Kusikiliza na Kutatua kero za Wananchi wa Kata ya Kyanyari na kueleza kuwa Utekelezaji wa huduma ya mtandao wa mabomba ya maji safi na salama umefikia asilimia 70 na kazi inaendelea.
Mhe. Sagini amesema Vijiji vyote vya Kata ya Kyanyari tayari vimefikiwa na huduma hiyo huku lengo madhumuni ikiwa ni kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji safi na salama kama alivyotoa ahadi kwenye majukwaa na mikutano mbalimbali na wananchi.
"Tumekubaliana sote kuwa tutazidi kuboresha na kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wote kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo," amesema Mhe. Sagini.
Naye Diwani wa Kata ya Kyanyari Mgingi Mhochi amesema kuwa Mbunge Sagini aliahidi kuwa Vijiji vya Nyakiswa, Mwibagi na Nyamikoma vya Kata ya Kyanyari vyote vitafikiwa na huduma ya mtandao wa maji safi na salama ambapo tanki la maji lita 150000 liliopo Mwibagi stoo linahudumia watu zaidi ya 20000 wa Kata ya kyanyari.
Pia Diwani Mgingi amemshukuru Mbunge Sagini kwa ushirikiano wake uliopelekea kuwezesha ujenzi wa miundombinu maji ya kisasa katika Kata ya Kyanyari iliyowezeshwa kupatikana sasa huduma ya maji ya bomba kwa wananchi.





Comments
Post a Comment