📍19 Machi 2025
🗒️ Dar es salaam
➖19 Mach 2021 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ilipata Raisi wa Kwanza mwanamke Shupavu na jasiri Muongoza njia. Ametimiza miaka minne Tanzania ikiwa na mafanikio makubwa.
➖Mungu kambariki Uwezo na ameweza kuivusha nchi. Amekuja na falsafa ya 4Rs na ametekeleza kwa vitendo.
➖Tanzania imefunguka kimataifa kaleta diplomasia ya Uchumi na kuvutia wawekezaji wa nje.
➖Ameleta demokrasia katika siasa na kufungulia mariadhiano baina ya vyama vya kisiasa na mikutano ya hadhara. Amefanya maboresho sheria za vyama vya kisiasa na ameunda tume huru ya.uchaguzi
➖Amefikia hatua za mwisho kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati SGR, Bwawa la Mwl Nyerere na daraja la Mwanza Kigongo- Busisi.
➖Ameboresha huduma za Jamii Afya Elimu, na Maji. Na ndio Champion wa Nishati safi kaleta hamasa kubwa katika utunzaji wa mazingira.
➖Katika afya amepunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
➖Elimu ameboresha miundo mbinu ya elimu, sera ya elimu na ameweka mkazo katika elimu ya ujuzi zaidi. Ujenzi wa vyuo vya veta katika kila halmashauri ili kukidhi upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi. Nakusisitiza matumjzi ya TEHAMA mashuleni. Na Ujenzi wa shule za Sayansi kwa wasicha na wavulana.
➖Amejikita kuwezesha wananchi kiuchumi Kupitia NEEC, mikopo ya 10% kwa halmshauri kwa makundi maalumu, mikopo kupitia wizara ya Ustawi na maendeleo jamii. Kaweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa.
➖ Ameanzisha Sera za kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na wananchi kwa ujumla.
➖Ameanzishwa sheria ya ulinzi kwa watoto dhidi ya Ukatili mitandaoni.
➖Ameboresha miundo mbinu ya barabara na bandari. Amenunua ndege mpya za abiria na mizigo.
➖Ameanzisha Samia legal aid ili kuleta utatuzika katika masuala ya kisheria kutatua migogoro ya Ardhi na nk.
➖ Ameanzisha matumizi ya TEHAMA katika Serikali E-Government na amesisitiza mifumo kusomana Mfano TRA, NIDA,RITA, BRELA, PPRA, na nk
➖Ameimarisha sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi.Viwanda na biashara, Madini na nk.
Kwa haya machache yaliyotajwa ameweze na ameweza tena huyu si mwingine ni
*Raisi Dakitari Samia Suluhu Hassan*
Mungu amlinde na kumbariki zaidi


Comments
Post a Comment