Serikali imesema watu 1,066 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani kati ya Julai 2025 hadi Aprili 2026, ikilinganishwa na vifo 1,275 vilivyotokea katika kipindi kama hicho mwaka 2024/25.
Takwimu hizo zimetolewa Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2026/27.
Amesema matukio ya ajali za barabarani yamepungua kutoka 1,322 hadi 1,233 katika kipindi hicho, hali inayoashiria maboresho ya usalama barabarani nchini.
Aidha, idadi ya majeruhi imepungua hadi 1,869 kutoka 2,278, sawa na upungufu wa asilimia 18.42.
Katambi amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi za Jeshi la Polisi katika kuimarisha doria, kusimamia sheria za usalama barabarani na kuchukua hatua kwa wanaokiuka sheria.
Serikali itaendelea pia kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili kupunguza zaidi ajali za barabarani.

Comments
Post a Comment