Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Tanga limejipanga kuendelea kutoa elimu Kwa wananchi ili kupunguza majanga na athari zinazoweza kutokea.
Hayo yamesemwa na kamanda wa Zimamoto na Uokoaji mkoani Tanga,Mrakibu mwandamizi Katala Issa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ameeleza kuwa ni jukumu lao kuhakikisha jamii wanafahamu matumizi sahihi ya nishati safi kama gesi na umeme.
Pamoja na hayo pia kamanda Katala pia amewataka wananchi kuoa taarifa mapema kupitia namba Yao ya dharura pindi wanapoona viashiria vya majanga na kutosubiri majanga kuwa makubwa kwani Kuna athari nyinge huzuilika kwani kwasasa jeshi lina mitambo mipya na yakutosha.
Sambamba na hayo pia amewataka kutumia vizuri namba hiyo kwani kumekuwa na watu wanaotoa taarifa za uongo na kuzua taharuki na kusababisha usumbufu Kwa jeshi hilo.
Jeshi la Zimamoto na uokoji pia limetaka wananchi kutojenga kiholela kwani hii huwapa wakati magumu pindi majanga yanapotokea.
"Sisi kama jeshi la Zimamoto na uokoji tunajukumu la kukagua kuanzia ramani mtu anapotaka kujenga na Kila hatua mpaka kukamilika Kwa jengo lakini watu hawafanyi hivyo sasa tunaomba wajenge Kwa kutumia wataalamna sio vishoka ili kujinusuru na majanga yanayoweza kutokea",alisema kamanda Katala.

Comments
Post a Comment