Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Watanzania 17 wameukana rasmi uraia wao baada ya kupata uraia wa mataifa mengine kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Sura ya 357 ya mwaka 2023.
Akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma leo Mei 25, 2026, Katambi amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria za uraia nchini.
Aidha, amesema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026, jumla ya wageni 64 walipewa uraia wa Tanzania baada ya kukidhi vigezo na taratibu zilizowekwa.
Pia amesema Watanzania 203 wamerejeshwa nchini kutoka mataifa mbalimbali baada ya kukiuka sheria za nchi husika, ikiwemo kuingia au kuishi bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Comments
Post a Comment