Watumishi wa Tume ya Madini washiriki Maadhimisho ya mei mosi kitaifa Njombe

GEORGE MARATO TV
0


📍Njombe

Watumishi wa Tume ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe wameshiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa Mei 1, 2026 katika Viwanja vya Lunyanywi, Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Maadhimisho hayo yanayofunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanahusisha wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali nchini waliokusanyika kuenzi mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya taifa pamoja na kujadili ustawi wao na kuboresha mazingira ya kazi.






Watumishi wa Tume ya Madini wameshiriki katika maandamano rasmi pamoja na taasisi nyingine za umma na binafsi, wakionesha mshikamano wa wafanyakazi wa Sekta ya Madini katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza uchumi kupitia rasilimali madini.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu isemayo, “Kazi zenye staha ni nguzo imara kwa maendeleo endelevu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050,” imelenga kuhamasisha ajira zenye heshima, kulinda haki za wafanyakazi na kuimarisha mchango wao katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya muda mrefu ya nchi.

Maadhimisho ya Mei Mosi hufanyika kila mwaka duniani kote kama jukwaa la kutambua mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kuhimiza mazingira bora na salama ya kazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top