Pandeni Miti Yenye Tija -Mtaka

GEORGE MARATO TV
0



Alvin Mushi - Njombe 

MKUU wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewataka wananchi  mkoani hapa kupanda miti yenye tija kama vile maparachiichi badala ya kupanda miti ya mapambo,

Bw Mtaka, ametoa wito huo wakati wa zoezi la upandaji miti uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mei Mosi 2026 ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani hapa.


Aidha amesema endapo kila mwananchi atapanda miti ambayo itamuongezea kipato kwanza atakuwa amekuza uchumi wake binafsi na taifa kuliko kuwa na miti ambayo faida yake ndogo.

“Miparachichi  ndiyo habari ya mjini yana soko kubwa ndani na nje ya nchi unaweza kupanda hata kuzunguka nyumba yako na ukapata faida kuliko kuwa na miti mingi ambayo inaishia kuwa mapambo” amesema Bw Mtaka




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top