Rais Ruto kulihutubia Bunge la Tanzania Mei Tano

GEORGE MARATO TV
0


 RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5, 2026, katika tukio linalotarajiwa kuvuta hisia za kisiasa na kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akisoma tangazo rasmi la Katibu wa Bunge leo Aprili 29, 2026, Naibu Spika, Daniel Sillo, amesema kikao hicho kitahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, huku hotuba ya Rais Ruto ikipewa uzito mkubwa kama sehemu ya mjadala wa siku hiyo.

Kwa mujibu wa Sillo, ujio wa kiongozi huyo unalenga kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya, hasa katika sekta za biashara, uwekezaji na maendeleo ya uchumi eneo ambalo limeendelea kuwa mhimili wa uhusiano wa nchi hizo mbili.

Tangazo hilo limetolewa katika Kikao cha 19 cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13 la Tanzania kinachoendelea jijini Dodoma.

Hotuba hiyo inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuonesha dira ya ushirikiano wa kikanda na kufungua fursa mpya za maendeleo kwa mataifa haya jirani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top