Rais Samia kuzindua Daraja la Kigongo - Busisi Juni 19

GEORGE MARATO TV
0

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua daraja la Kigongo- Busisi (KM 3) juu ya Maji linalounganisha wilaya za Misungwi na Sengerema juni 19 mwaka 2025.

Waziri wa Ujenzi mh Abdallah Ulega ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika katikati ya daraja hilo alipokua akielezea kazi zilizotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.

Amebainisha kuwa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi imefanikiwa sana kwenye ujenzi wa madaraja, barabara, vivuko na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii pamoja na kukuza uchumi wa watanzania.

Ulega amesema pamoja na kukamilika kwa daraja hilo lililogharimu Bilioni 716, serikali ya awamu ya sita imejenga madaraja mengine mengi kama Tanzanite (KM 1) juu ya bahari, Wami (Mita 510), Kitengule (140 Mita), Msingi- Singida (Mita 100).

Amesema, daraja la Kigongo Busisi limejengwa na kampuni ya CCECC kwa kushirikiana na wataalamu wazawa ambao ni wabobevu kwenye kazi hizo na kwamba nchi za jirani wajiandae kwa neema ya barabara hiyo.

Aidha, amebainisha kuwa daraja hilo lina uwezo wa kupitisha magari zaidi ya elfu 20 kwa siku na kwa dakika 3 hadi 5 tu gari itakua imeshavuka kutoka upande mmoja na mwingine.


Vilevile, amefafanua kuwa kwa umahiri wa Rais Samia amefanisha kukamilisha daraja hilo ambalo wakati anaingia madarakani lilikua limejengwa kwa asilimia 25 tu lakini serikali yake imekamilisha asilimia 75 zilizobaki kwa kulipa zaidi ya Bilioni 500.

Vilevile Waziri Ulega amebainisha uwezo wa daraja hilo kuwa lina uwezo wa kubeba gari zenye uzito usiozidi tani 160 kwa wakati mmoja sawa na magari manne yenye tani zaidi ya 45 na amewataka wananchi kulinda rasilimali za daraja hilo na miundombinu mingine kwa manufaa ya watanzania wote.

Sambamba na madaraja amefafanua kuwa mtandao wa barabara umeongezeka kutoka Kilomita elfu 36 hadi 37. 4 kutokana na kupandishwa kwa hadhi ya barabara kutoka wilaya kwenda kuwa za mikoa huku akizitaja barabara za Mbambabay (KM 66), Kigoma-Kasulu (KM) 100.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top