Msama Awajia Juu Viongozi Wa Dini Wanaotumia Nyumba za Ibada Kuvuruga Amani

GEORGE MARATO TV
0


Mkurugenzi wa Msama promotion ALEX MSAMA amewataka viongozi wa dini nchini kuacha mara moja vitendo vya kutumia nyumba za ibada kuwa sehemu ya kuhubili siasa kwa baadhi yao nchini.

Hayo amebainisha hio leo Juni 08, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa kitendo cha viongozi hao ni kuikosea serikali na ni kitendo kisichofaa na ni kushindana na agizo la Mungu na kwani kufanya hivyo ni kumkosoa mungu kupitia tabia zisizo za kiungwana za kutoheshimu mamlaka za serikali na miimili yake.

Aidha, Msama amesema kuwa yote yanayofanyika na Rais samia Suluhu Hassan ni maerekezo ya Mwenyezi Mungu hivyo ni busara kutii mamlaka ya serikali kwani kile kinachofanyika na Rais ni hitajio la mungu kwa watanzania.

Hata hivyo pia Msama ametoa rai kwa watanzania kuacha kutumia lugha za matusi na zisizofaa mitandaoni na katika jamii, kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha mmomonyoko wa maadili huku akilitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua wote wanaotumia lugha zisizofaa mitandao kwa kutukana viongozi na wasiokuwa viongozi .

 Msama amewasihi viongozi wa dini na watanzania kutii mamlaka ya za serikali kwani uwepo wa mamlaka hizo ni hitajio la mwenyezi mungu katika dunia hii jambo ambalo ameshalizungumza katika vitabu vya kidini.

Katika hatua nyingine Msama amewashauri viongozi wa dini nchini kuachia ngazi nafasi zao za kidini ili kushiriki siasa kwani kitendo cha kuchanganya siasa na dini huwenda kikachochea hali isiyofaa katika jamii.

Watanzania wanapaswa kutambua umuhimu wa mamlaka na kazi zake na kuhabarishana madhara juu ya maswala kadhaa kuhusu kuchanganya siasa na dini katika madhabahu kwa kujenga demokrasia bora na amani ya taifa la Tanzania.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top