Waziri mkuu mstaafu mh Mizengo Peter Pinda ameongoza kikao cha Bodi ya Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kilichofanyika leo juni 08 mwaka 2025 Jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho mh Pinda amezungumzia umuhimu wa kulinda amani ikiwa ni sehemu kumuenzi mwasisi wa Taifa la Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere, na kuendelea kuyaenzi mazuri yote tulioachiwa na Baba wa Taifa ikiwa ni pamoja na kupinga rushwa hasa katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani.