Mwandishi, mwanamageuzi mtajika Ngugi wa Thiong’o aaga dunia

GEORGE MARATO TV
0

Mwandishi wa Riwaya  mtajika duniani na mwanamageuzi Ngugi wa Thiong’o ameaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu nchini Marekani, familia yake imethibitisha.

Bw Ngugi ambaye anachukuliwa kuwa mwandishi mahiri zaidi wa riwaya Afrika Mashariki amekuwa nchini Marekani kwa miaka mingi na katika miaka ya hivi punde amekuwa akilemewa na maradhi.

Ripoti zinasema alikufa kwa mshtuko wa moyo.

Mwanawe, Mukoma wa Ngugi, aliandika kwenye safu yake mtandaoni:

“Nimejawa na majonzi kusema kwamba babangu, Ngugi wa Thiong’o alikata roho Jumatano, Mei 28, 2025,Ningekuwa mimi nilivyo kama mwanawe, msomi na mwandishi bila yeye. Nampenda. Sijui itakavyokuwa kesho. Hayo tu ndio naweza kusema kwa sasa"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top