Machi 30, 2025 Mbunge wa Njombe mjini mhe. DEO MWANYIKA (MB) ametoa mahitaji ya sikukuu ya Idd El Fitri inayotarajiwa kufanyika Machi 31, 2025 kwa wazee na wahitaji katika misikiti yote ya Njombe mjini.
Akiongea wakati wa kukabidhi mahitaji hayo Mhe Mwanyika amewapongeza waislamu wote kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao unakwenda kuhitimishwa kwa sikukuu ya Eid Machi 31, 2025.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Njombe amemshukuru Mhe. Mbunge kwa majitoleo yake kwa waislamu wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwani amekuwa akichangia mahitaji ya mfungo kila mwaka. Waislamu wanamtakia heri na baraka katika majukumu yake aliyokabidhiwa ya kuwatumikia wananjombe na watanzania kwa ujumla.







Comments
Post a Comment