Na Shomari Binda-Bunda
MKURUGENZI wa kampuni ya Audacia Investment Ltd na mdau wa Maendeleo wilaya ya Bunda mkoani Mara Bw Kambarage Wassira amefanikisha kupatikana kwa shilingi milioni kumi za kusaidia Maendeleo ya kanisa la Waadventista Wasabato Nyasura juu mjini Bunda.
Bw Kambarage Wasira ambaye pia ni kada wa CCM aliwakilishwa katika harambee hiyo kama mgeni rasmi na Safari Lubulila ambapo alichangia shilingi milioni moja Taslimu.
Akizungumza kwenye harambee hiyo Kambarage amesema viongozi wa dini kupitia nyumba za ibada wanasaidia kujenga maadili kwenye jamii hivyo ni muhimu kujenga na kuziimarisha.
Amesema ili taifa liweze kusonga mbele kwenye maendeleo jamii wakiwemo vijana wanapaswa kuwa na maadili mema na viongozi wa dini wamekuwa msaada kwa serikali eneo hilo.
Kambarage ambaye amekuwa mstari wa mbele kuchangia masuala ya jamij mara kwa mara kwenye kwenye matukio tofauti ametoa wito kwa kila mmoja kuchangia kwenye mambo ya dini.
" Niko hapa kumuwakilisha ndugu yetu mdau wa maendeleo Kambarage Wasira katika kuimalisha ujenzi wa nyumba ya Mungu.
" Kutokana na majukumu mengine ya kijamii ameshindwa kufika lakini yupo pamoja na nasi na amechangia kiasi cha shilingi milioni moja",amesema Safari
Katika harambee hiyo mdau mwingine wa maendeleo wilayani Bunda Willison Mukama amechangia kiasi cha shilingi 500,000.
Mchungaji wa Kanisa hilo Mukama Sagati umewashukuru wachangiaji wote na kuiomba jamii kuchangia nyumba za ibada
Amemshukuru pia Kambarage Wasira kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kuemdesha harambee hiyo na kufanikisha kupatikana kiasi cha shilingi milioni 10.
"Tunamshukuru sana Ndugu yetu Kambarage Wasira amekuwa ni baraka kwa kanisa la Wasabato Nyasura awamu ya kwanza tulimpa mwaliko akiwa mgeni mwalikwa aliitika na kutuchangia shilingi 2,000,000 na awamu hii pia ametenda kwa kutoa kiasi cha sh 1,000,000"alisema na kuongeza
"Kanisa linashumshukuru sana tunamuombea kwa Mungu aendelee kumpa moyo huo na kumfanikishia katika shughuli zake"alisema mchungaji Sagati.

.jpg)

.jpg)




Comments
Post a Comment