Ni "Upuuzi" Kumdai Mh Waziri Mkuu Majaliwa Maendeleo ya Wana-kusini Pekee!

GEORGE MARATO TV
0


Nimesoma andiko moja kwenye mtandao wa Jamii Forum ambalo naweza kuliita andiko la "kipuuzi" sana ambalo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwani linajenga picha kuwa Viongozi wetu wa ngazi za kitaifa wanawajibika kupendelea maeneo yao(kwao)kwanza kabla ya maeneo mengine ya Nchi!


"Waziri Mkuu Ana "Legacy " Gani ya Kujivunia Kwa Watu wa Kusini?"

Kwa kumbukumbu zangu,karibia mwezi wote March,2025,Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekuwa katika ziara za mikoani katika kuwahudumia Watanzania wote kwa Ujumla wao!Sijui ni lini Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa amefanya ziara ya Kiserikali/Kikazi Mkoani Lindi au Mtwara!

Ndani ya wiki moja hii Waziri Mkuu Majaliwa nimemuona kupitia TV katika Mikoa ya Tabora badae Mkoani Njombe na leo alikuwa Mkoani Kilimanjaro!Sitoshangaa kesho nikisikia yupo Dodoma au Mkoani Katavi au Kigoma!


Nini NATAKA KUSEMA?

Mh.Waziri Mkuu ni moja wa viongozi wanne wa juu kabisa kwenye ngazi ya Kitaifa!Mh Waziri Mkuu kabla ya yote kwanza anawajibika kwa Watanzania wote katika kusimamia Maendeleo ya Taifa akiwa kama Mtendaji Mkuu wa Serikali akimsaidia Mh Rais,Mama Samia Suluhu Hassan!

Huyu sio Waziri Mkuu wa Wamakonde wala Wamwela au Wamakua!Huyu ni Waziri Mkuu ndani ya kona zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Pili,Kama Mzee hayati Benjamin Mkapa,Rais wa awamu ya tatu wa JMT angekuwa na akili kama za Mwandishi(Nandagala One- wa Mpumalanga)basi ni wazi tangia "juzi" Kusini ingekuwa kama Ulaya!Mpaka Mzee Hayati Benjamin Mkapa anafariki dunia barabara ya kwenda nyumbani kwake kijijini Lupaso Mkoani Mtwara ilikuwa haina lami!Mpaka sasa kule nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya milimani hakuna lami!

Barabara ya Singida- Katesh-Hanang ambako ndiko alikokuwa anatoka Waziri Mkuu wa awamu ya tatu,Mzee Fredrick Sumaye mpaka anastaafu(PM)barabara hiyo ilikuwa haina lami na NGUMU kupitika mvua ikinyesha!

Tatu,Uwaziri Mkuu wa Mh Kassim Majaliwa principally unatokana na Ubunge wa Ruangwa kwanza!Mh Waziri Mkuu Majaliwa kabla ya kuutumikia "Uwaziri Mkuu" ni lazima sana atumikie sana kwa Wananchi wake wa Jimbo la Ruangwa ambao ndio kimsingi walimchagua kwa kura!

Ni makosa makubwa kumpima Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kigezo cha ukanda(Kusini) lakini Mh Waziri Mkuu huyu huyu anapaswa kupimwa kama Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kwanza!Mh Nape Mnauye pia anapaswa kupimwa kwa Jimbo lake la Mtama na hivyo hivyo kwa Kaptain Mstaafu Mh George Mkuchika anatapimwa kwa kigezo Jimbo lake la Newala na sio uwaziri wake au "ukanda" wake!

Mwacheni Mh Waziri Mkuu atoe huduma yake kwa Watanzania wote na kamwe asipewe shinikizo la "kikanda"(Kusini)sababu tu anatoka Kusini kwani Tanzania yote ni ya kwake katika kusimamia kutoa huduma kwenye sekta ya Maji,Barabara, Afya,Kilimo,Uvuvi na sekta zinginezo!


Huyu ni miongoni mwa Mawaziri Wakuu bora sana kuwahi kutokea ndani ya Nchi hii!Angalia๐Ÿ‘‡๐Ÿฟ๐Ÿ‘‡๐Ÿฟ


Mradi mzuri wa SGR ulianzia mgongoni mwake akiwa na hayati John Pombe MAGUFULI na Samia Suluhu Hassan na imekamilika kutokea Dar -Dodoma ndani ya Uwaziri Mkuu wake akiwa na kiongozi wake Mkuu,Mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan!

Bwawa la Mwalimu Nyerere(MW 2000+)limekamilika yeye akiwa msimamizi Mkuu kwa maana ya Wizara zote za Serikali hii huku akiwa na Kiongozi wake Mkuu,Mh Rais Samia Suluhu Hassan!

Lakini sijui Watanzania wangapi wanajua kuwa hiyo "Midege" ya ATCL kuifufua ilikuwa ni mawazo ya JPM,Mama Samia pamoja na Waziri Mkuu wao(Kassim Majaliwa )!Miradi yote mikubwa ndani ya Serikali ya awamu ya tano na Sita ina mkono wa Waziri Mkuu Majaliwa sababu ya nafasi yake ya Waziri Mkuu!

Huyu Kassim Majaliwa Majaliwa ni mmoja kati ya wazalendo wachache ambao Taifa linajivunia kwa wakati huu!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top