Rais Samia Atoa Mkononl Wa Pole Milioni Mia Kwa Wananchi Walioathiriwa na Mvua Mjini Musoma

GEORGE MARATO TV
0


RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan atoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya wananchi waliothiriwa na mvua ilionyesha juzi usiku na kusababisha maafa makubwa katika baadhi ya maeneo ya mji wa Musoma.

Mkuu wa mkoa wa Mara kanali Evans Mtambi amepokea kiasi cha fedha ili kiweze kuwasaidia wananchi ambao wamekumbwa na janga hilo.

Katika tukio hilo zaidi ya kaya mia tatu zilikosa makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa na nyingine kubomolewa,huku majengo ya taasisi kama shule na miundombinu ya umeme na simu vikiathiriwa na mvua hiyo iliyoambata na na upepo mkali usiku wa kuamkia machi 23 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top