Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Nilijiapiza kujenga shule ya Msingi Misufini bila fedha ya serikali


📍 Asema nadhiri aliyoweka ilitokana na watoto kusoma umbali mrefu

📍 Asema alipokosa fedha serikali alianzisha msalagambo kusaka marafiki zake kutimiza nadhiri yake

📍 Awashukuru CRDB Benki, Karimjee Foundation kumsaidia kujenga madarasa mawili na vyoo

📍 CRBD yaungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumpongeza MwanaFA kwa kazi nzuri anayofanya Muheza 

📍 Mtendaji wa Kijiji Ataka umbali waliokuwa wakisoma watoto wa Kijiji cha Misufini 

📍 Wazazi Misufini Wasema hawakukosea kumchagua MwanaFA kuwa mbunge, wamtaja pia Rais 


Na Mwandishi Wetu, Magoroto 

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA, alisema alijiapiza na kuweka nadhiri ya kujenga shule ya msingi katika Kijiji cha Misufini kilichopo kata ya Magoroto kilichokuwa kikikabiliwa na changamoto lukuki.

Sambamba na nadhiri hiyo, MwanaFA hakutegemea kama wananchi wa Kijiji hicho wangekichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa walikabiliwa na changamoto nyingi.

Alisema Kijiji hicho kilikuwa kikikabiliwa na tatizo la ukosefu wa Maji, Umeme, shule na barabara ambazo sasa tangu awe mbunge, huduma zote hizo amewafikishia.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa shule shikizi iliyojengwa na wahisani wake, Benki ya CRDB Machi 26 2025, MwanaFA alisema alijua matatizo hayo alipokwenda kufanya kampeni kuomba kura za Rais, Diwani na Mbunge mwaka 2020.

Alisema alifika katika Kijiji hicho Septemba mwaka 2020 kuomba kura akiwa na wenzake, lakini walilazimika kuacha magari katika Kijiji cha Gare kutokana na Kijiji hicho kukosa barabara ya kufika makao makuu ya Kijiji hicho.

Alisema alipofika katika Kijiji hicho walifanya mkutano na kundi la watoto wa shule waliwasindikiza kurudi Gare huku wakiwaambia nyimbo mbalimbali.

Alisema wale watoto aliwauliza "kwanini nyie hamchoki, wakasema wao Kila siku wanaenda na kurudi Gare kwenda kusoma. 

Alisema kitendo cha watoto wale kuwasindikiza walitumia falsafa ya kumfikishia ujumbe kwamba wanauhitaji mkubwa wa kupata shule ili wasome karibu na nyumbani kwao.

"Kwahiyo Mimi nikajiapiza, nikaweka nadhiri ya kwamba moja ya mambo nitakayofanya ni kuwajengea shule wapate elimu yao hapa Kijijini kwao," alisema.

MwanaFA alisema baada ya kuchaguliwa aliulizia halmashauri kuona uwezekano wa kujenga shule katika Kijiji hicho lakini halmashauri hawakuwa na bajeti.

"Nikaamua kufanya msalagambo wa kuwatafuta marafiki zangu kuhakikisha shule hii inajengwa, nawashukuru ndugu zangu wa CRDB kwa kunisaidia kujenga madarasa mawili na matundu sita ya vyoo," alisema.

Alisema watu wengine waliomjengea madarasa mawili ni Richard Karimjee kupitia taasisi yake ya Karimjee Foundation nao pia aliwashukuru na yeye mwenyewe amejenga madarasa mawili. Jumla shule hiyo ina vyumba sita.

Mbunge huyo wa Muheza, alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya hiyo, Dkt Jumaa Mhina kuhakikisha anaipatia walimu shule hiyo ili watoto hao waweze kusoma jirani na Kijiji chao lakini pia kutengeneza barabara kutoka katika shule hiyo hadi Kijijini.

Akizungumza katika hafla hiyo Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya benki ya CRDB, Miranda Mpogolo alisema shule hiyo wameijenga kwa gharama ya shilingi milioni 66.1 kupitia sera yao ya kusaidia jamii.

Alisema kuwa benki hiyo imeandaa sera maalum ambayo inasaidia jamii katika miradi ya Elimu, Afya na mazingira ambapo kwa mwaka jana pekee walitumia zaidi ya shilingi bilioni 2.3 kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii nchini.

Alisema walipopokea ombi la mbunge wa Muheza waliguswa sana na hata pale alipomwambia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara wilayani Muheza waliona umuhimu mkubwa wa kujenga shule hiyo.

"Tunakupongeza mhe mbunge kwa kazi nzuri unaiyofanya hapa Muheza, tumeona Rais akiwa Muheza kwenye ziara yake alikupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya, na sisi CRDB benki ni mashuhuda na tunaungana naye kwa pongezi hizo, tunakupongeza sana," alisema Mpogolo.

Akisoma taarifa fupi Mtendaji wa Kijiji cha Misufini Pius Emanuel alimshukuru mbunge kwa kufanikisha upatikanaji wa shule hiyo akieleza kwamba umewasaidia watoto kuepukana na umbali mrefu wa kufuata shule.

Alisema watoto 100 walikuwa wakitembea umbali wa kilomita 12 kwenda na kurudi katika shule ya msingi Gare na wanafunzi wengine 60 walilazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule ya msingi Tongwe.

"Wanafunzi wengi waliacha shule kutokana na umbali huo, wasichana walikatisha ndoto zao hivyo hili ulilolifanya mheshimiwa mbunge ni jambo kubwa ambalo tunahitaji kukuunga mkono," alisema mtendaji huyo.

Katika risala ya wazazi iliyosomwa na wanafunzi walisema jambo ambalo mbunge huyo amelifanya kiukweli watamuunga mkono kutokana na ahadi zake kuwa za kweli.

"Sisi hatukukosea kukupa ubunge lakini pia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hajakosea kukuteua kuwa Naibu Waziri unastahili kwasababu ni kiongozi unayetatua changamoto zetu kwa uhakikika hongera sana," ilisema risala hiyo.












Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...