No Reforms No Election Mara, Ujumbe Wafika Kwa Baba Wa Taifa

GEORGE MARATO TV
0



Na Shomari Binda-Butiama

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa mara Mwalimu Chacha Heche amefika kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na ujumbe wa viongozi wa mkoa na wilaya ya Butiama.

Kiongozi huyo amefanya mazungumzo na familia ya Baba wa Taifa ikiwa ni pamoja na kutambulisha uongozi mpya wa Chadema mkoa wa Mara kwa familia hiyo.

Licha ya kutambulisha uongozi amewasilisha vielelezo vya matukio yaliyojitokeza katika chaguzi za Tanzania 2019-2024 mkoa wa Mara 

Katika taarifa aliyowasilisha Mwenyekiti huyo imesheheni vielelezo vya mauaji kwenye chaguzi,utekaji kwenye chaguzi,majeruhi,kura fake,ubambikaji kesi nyakati za uchaguzi ,ukiukwaji was sheria nyakati za uchaguzi na uenguaji hovyo wa wagombea.

" Tunashukuru kwa mapokezi ambayo tumeyapata hapa nyumbani maana hii ni familia yenye heshima kwenye taifa letu.

" Tumekuja kutambulisha uongozi wa mkoa wa chama pamoja na Wilaya ya Butiama pamoja na kuzungumzia masuala ya kisiasa na masuala ya kijamii ndani ya taifa"amesema.

Mwakilishi wa familia ya Baba wa Taifa Madaraka Nyerere amepokea amepokea taarifa ya chama hicho kwa mikono miwili na kuushukuru uongozi wa chama hicho kuwafikia na kufanya mazungumzo.

Amesema mazungumzo ya pamoja yana tija katika katika kutafuta suruhisho la masuala mbalimbali yakiwemo ya kisiasa na maendeleo.

Ujumbe huo wa Viongozi wa Chadema Ukiwa Mwitongo pia umepata fursa ya kutoa Heshima kwenye Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 

Mapema kabla ya kufika kwenye familia hiyo Mwenyekiti huyo wa Chadema mkoa wa Mara amezuru na kuwasilisha taarifa kwa uongozi wa makanisa ya kipentekoste Tanzania (CPCT-Mara)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top