Na Mwandishi Wetu, Kagera
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema ilani yake ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, itakuwa na majawabu ya changamoto mbalimbali za vijana ikiwemo namna ya kutatua changamoto ya ajira.
Hayo yameelezwa leo Machi 22, 2025 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kemondo, Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuimarisha uhai wa Chama.
Amesema kuwa Chama kinafahamu changamoto ambazo vijana wanakumbana nazo na kwamba Ilani ijayo ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, itakuja na majibu ya shida zao.
“CCM inajua matatizo ya vijana, na imekuwa na mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto za vijana. Kwanza CCM imenzishwa na vijana kwani Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na miaka 32)
“Lakini hakuna chama cha wazee peke yao labda kiwe chama cha wazee, lakini chama cha siasa lazima kiwe Ccm Kuja na Ilani ya Kutatua Changamoto za Vijana - Wasira vijna, kijue matatizo ya vijana na kutafuta ufumbuzi wake,” amesema Wasira.
Amefafanua katika kutatua changamoto za vijana CCM kupitia Ilani yake ijayo ya Uchaguzi Mkuu itakuja na majibu ya matatizo ya vijana kutafuta ufumbuzi wake na kusisitiza katika Ilani inayokuja imekubalika vijana ni lazima wapewe nafasi.





Comments
Post a Comment