Tumepata heshima ya kukaribishwa na Mh. Raila Amolo Odinga ofisini kwake jijini Nairobi kwa ajili ya mazungumzo juu ya hali ya kisiasa nchini kwetu na harakati za mapambano ya kidemokrasia zinazoongozwa na chama chetu.
Tumepata fursa ya kumweleza RAO juu ya msimamo wetu wa 'No Reform No Election' na kupata uzoefu na ushauri wake.
Kama jina lake la utani linavyoashiria, RAO ni 'Baba' wa kweli wa demokrasia katika ukanda wetu wa Afrika. Pamoja na baba yake, Mzee Jaramogi Oginga Odinga, RAO alikuwa mfungwa wa kisiasa wa mara kwa mara wa tawala za Mzee Jomo Kenyatta na Daniel arap Moi.
Licha ya mateso mengi na makubwa akiwa kizuizini katika magereza mbalimbali ya Kenya, 'Baba' hakuwahi kukata tamaa wala kusaliti harakati za kudai demokrasia nchini kwake.
Na Leo tumejua kutoka kwake tulichokuwa hatukijui kabla: alipatiwa passport yake ya kwanza mwaka 1962 (akiwa na umri wa miaka 15!) na Serikali ya Tanganyika baada ya serikali ya kikoloni ya Kenya kumnyima yeye na kaka yake nafasi za kusoma nchini kwao kutokana na siasa za upinzani dhidi ya ukoloni za baba yao, Jaramogi Oginga Odinga!
Passport hiyo ilitolewa kwa amri ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, baada ya Jaramogi na watoto wake hao kutorokea Tanganyika ili waweze kwenda masomoni nchini Ujerumani Mashariki ya miaka hiyo.
Ama kweli Afrika Mashariki ina deni kubwa kwa shujaa huyu wa demokrasia kwa mfano wa maisha yake ya harakati

.jpg)
.jpg)


Comments
Post a Comment