Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amemfuta kazi Balozi wa nchi hiyo,Nchini Afrika Kusini Baalizi Mazuba Monze.
Hichilema amechukua uamuzi huo baada ya Monze kuripotiwa kutaka wafanyakazi wake wa kiume kumnyoa sehemu za siri.
Mwanadiplomasia huyo aliyekuwa akihudumu katika ubalozi wa Zambia mjini Pretoria ameripotiwa kuwataka wafanyakazi wa ubalozi kumnyoa sehemu za siri ambapo wafanyakazi hao walikataa,wakisema kuwa haikuwa sehemu ya majukumu yao kumnyoa Balozi sehemu za siri.
Balozi Monze alichukuliwa kitendo hicho kuwa ni kutotii na hivyo kupelekea kuwafuta kazi.
Hata hivyo baada ya ukimya wa muda mrefu, wafanyakazi hao walikataa rufaa dhidi ya uamuzi huo na kulifikisha suala hilo kwa wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wakati madai hayo yaliyowashangaza wengi yalipothibitishwa,Rais Hakainde Hichilema alimfuta kazi mara moja Balozi huyo huku ripoti nyingine zikisema kuwa madai dhidi ya Monze yametiwa chumvi.
Gazeti la Maravi Post linaripiti kuwa rais wa Zambia anayeishi Afrika Kusini amejitokeza akidai kuwa madai dhidi ya Monze huenda yametiwa chumvi au Kutungwa na wapinzani wake,Mtu huyo anadai kuwa kampeni ilizinduliwa dhidi ya Monze,ikihusisha ripoti za uongo na uzushi ambao hatimaye ulisababisha kufukuzwa kwake.
Wakati hayo yakiendelea bado inabakia kusubiriwa ni hatua gani zaidi zitachukuliwa na Matokeo gani Monze atakabiliana nayo.
Hata hivyo, Jambo moja ambalo ni hakika ni tukio hilo limeacha doa kwa sifa ya kidiplomasia na kuibua maswali Juu ya Mwenendo wa wawakilishi wake nje ya nchi.