Maneno hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu wakati akifunga mafunzo ya Watumishi wa Serikali, Mahakama na Taasisi za Umma yaliyodhaminiwa kwa ushirikiano wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Taasisi ya OSHA inayosimamia Usalama na Afya mahala pa Kazi, yaliyofanyika katika ofisi za OSHA,Dodoma.
Katika mkutano huo, Kikwete amewakumbusha umuhimu wa kuzingatia mafundisho waliyoyapata na kuendelea na mapambano ya kupinga unyanyasaji dhidi ya watu wenye Ulemavu.
Pamoja na hilo Waziri huyo wa Kazi amewapongeza Mahakama kwa kutoa kipaumbele kwa wenye Ulemavu katika kada zote za kiutendaji ndani ya Muhimili huo wa Nchi. Pamoja na salamu hizo Waziri wa Kazi aliwakumbusha watendaji hao hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya Sita katika kuhakikisha Haki na Maslahi ya Wenye Ulemavi yanasimamiwa kwa kutunga sera na mipango mbalimbali ikiwemo inayowezesha Sera hizo kutekelezeka.