Kazi njema na ya Kizalendo inayofanywa na Mpc yamgusa Dc Ngubiagai

GEORGE MARATO TV
0



Na Obunde Michael;Mwanza

Waandishi wa habari mkoani Mwanza wameaswa kutumia Uhuru wa habari uliopo nchini kuandika na Kutangaza habari zenye tija ili kuimarisha ustawi wa Jamii pamoja na kuchochea maendeleo ya kijamii na Kiuchumi. 

Mkuu wa wilaya Ukerewe Christopher Ngubiagai ametoa wito huo Jijini Mwanza wakati wa hafla ya usiku wa waandishi wa habari na wadau wa habari mwaka 2024.


Ngubiagai aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza Said Mtanda kwenye hafla hiyo amesema kuwa vyombo vya habari vina Jukumu la Kutoa Taarifa kwa usahihi pamoja na kuzingatia maslahi mapana ya umma kwenye kila hatua ya kutoa habari. 

"Mi binafsi Nina furaha kubwa kumwakilisha Mkuu wetu wa Mkoa katika Tukio hili muhimu ambalo linaadhimisha mchango wa vyombo vya habari katika maendeleo ya Jamii yetu na Taifa kwa Ujumla,Lakini kwanza kabisa natoa pongezi za dhati kwa chama cha waandishi wa habari Mkoa Mwanza (MPC) Nawapongeza Sana kwa kazi kubwa,njema na ya kizalendo mlioifanya kwa miezi yote 12,hongereni sana"alisema Ngubiagai na kuongeza kuwa

"Vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika kuhakikisha kuwa raia wanapata habari sahihi,wanashirikishwa kwenye Mambo ya kijamii na wanapata fursa ya kutoa maoni yao,Uhuru huu unahakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi yao bila kuogopa wala kuingiliwa na bila kutumika na mtu yoyote kwa maslahi ya upande mmoja"

Naye Mwenyekiti wa MPC Edwin Solo amesema Tasnia ya habari itaendelea kufanya kazi kwa misingi ya sheria na weledi. 


"Kuna wakati kuna miiko ya uandishi wa habari na kuna wakati kuna sheria na inapotokea mgongano wa namna hiyo, sheria za nchi huwa zinatangulia,hivyo tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria za nchi sanjari na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari, pia dhamira yetu ni Kuhakikisha uandishi wetu wa habari unakuwa ni wa kutatua matatizo,Tunaita solution Journalism"alisema Soko

Hafla imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Tasnia ya habari ikiwemo Takukuru,Nhif,Nsssf,Pssf na Tashico ambao wameahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika utekelezaji wa majukumu hao.






Wadau hao wameomba wanahabari kuendelea kuandika na Kutangaza shughuli zinazofanywa na Taasisi zai ikiwemo kuhamasisha waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya pensheni ili kuwezesha mifuko hiyo kulipa pensheni kwa wakati muafaka. 

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Meli Tanzania(Tashico) Eric Hamisi amesema mabadiliko yaliyofanyika kwenye kampuni hiyo yakiwemo ya Jina yamelenga Kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma. 

Hamisi amesema kuwa malengo hayo yatafikiwa ikiwa wanahabari wataendelea kuandika mema yanayofanywa na kampuni hiyo pamoja na kuhamasisha wananchi kutumia huduma zinazotolewa. 
















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top