Uadlifu ni kipimo cha mtu kuchaguliwa kiongozi

GEORGE MARATO TV
0

 

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Christopher Ngubiagai ambaye ni Mgeni Rasmi kwenye mafunzo ya Viongozi wa CCM amesema Chama hicho kitaendelea kutawala kwa sababu wanaoomba kutawala bado hawajajiandaa, akawasisitiza vijana kujiandaa vyema kwani ndio viongozi wa kesho.

Amesema vijana wasomi wa Tanzania wanapaswa kuwa wazalendo, ili Taifa liwe na rasilimali watu watakaoisaidia nchi yetu kwa ustawi wa vizazi vyetu

"Kijana ili awe Kiongozi bora anapaswa kuwa na ari ya kujifunza na kuleta mabadiriko, bila kusahau nia ya kweli ya kuwatumikia watanzania, sambamba na kushiriki katika kuleta maendeleo, Ujana sio umri bali ni fikra za kujipambanua katika kufanya kazi ili kuleta maendeleo" - DC Ngubiagai

Aidha amesema, vijana hawapaswi kuwa watazamaji bali kuwa mstari wa mbele katika kujenga Taifa letu na kuongeza kuwa ukabila ni sumu ya maendeleo kwa maana inaweza kuchelewesha maendeleo na uzalendo.

"Kiongozi thabiti anayefaa anapaswa kuwa muwajibikaji, mwadilifu, mbunifu,, msikivu na Mzalendo na akaongeza "vyombo vya habari vinajukumu la kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu uzalendo" DC Christopher Ngubiagai





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top