Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amepewa tuzo na Chuo Kikuu cha Iringa kwa kutambua na kuthamini ushirikiano mkubwa na kujitoa kwake katika kuchangia mafanikio na ukuaji wa Chuo hicho.
Tuzo hiyo iliyotolewa tarehe 13 Disemba 2024 imekabidhiwa kwake leo tarehe 17 Desemba 2024.
Jenerali Mkunda amekishukuru Chuo hicho kwa kupewa heshima ya kustahili tuzo hiyo na kuthamini mchango wake kwa niaba ya JWTZ.
Jenerali Mkunda ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Chuo hicho na JWTZ.

.jpg)
.jpg)
.jpg)