Benki Kuu ya Tanzania Yaainisha Sababu za Kuimarika Kwa Shilingi

GEORGE MARATO TV
0

 


Benki kuu ya Tanzania(BOT) imebainisha  sababu mbalimbali zilizochangia kuimarika Kwa Shilingi kuwa ni pamoja na usimamizi mzuri wa Sera ya Fedha ambapo katika robo ya 4 ya mwaka 2024, BoT ilitangaza riba ya asilimia 6 ili kupunguza ukwasi wa shilingi zilizokuwa nje ya shughuli za kiuchumi. 

Akizungumza na GMTV,Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba ametaja Sababu nyingine kuwa ni Kudhibitiwa Kwa magendo katika soko la fedha za kigeni (fx black market) na kupunguza uwezekano wa kununua fedha za kigeni zinazohodhiwa kwa ajili ya kuziuza baadaye kwa bei ya juu (fx speculation)


BoT pia imeendelea kudhibiti Taasisi za Serikali, wafanya biashara na watu binafsi kutoza au kuuza bidhaa na huduma za ndani kwa kutumia fedha za kigeni ili kupunguza mahitaji yasiyokuwa ya lazima ya fedha za kigeni nchini, kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha sheria ya BoT. 

Aidha Kumekuwepo na Ongezeko la mauzo nje (dhahabu, korosho, kahawa, mchele, mahindi, ufuta, mbaazi, dengu, choroko, n.k); kuongezeka kwa bidhaa na huduma za utalii; kupungua kwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa hizo nchini (mafuta ya kula, sukari, vioo, vigae/marumaru, mbolea, vifaa vya ujenzi, n.k.); 

 Kwa Mujibu wa Gavana Tutuba, ongezeko la Uzalishaji wa umeme uliopunguza matumizi ya mafuta ya nishati nchini; kuimarika kwa uchumi wa dunia uliosababisha kupungua kwa bei za bidhaa zinazoagizwa nje pamoja na gharama za usafitishaji hususan wa meli; na kupungua kwa mfumuko wa bei wa nchi zilizoendelea nalo limechangia kupungua kwa riba ya benki kuu katika nchi hizo na hivyo kuongeza ukwasi wa fedha za kigeni duniani.



Mwaka jana BoT ilianzisha programu ya Export Credit Guarantee Sceheme ili kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni nchini kupitia export promotion and import substitution initiatives ambapo baadhi ya sekta zimeanza kuongeza uzalishaji na thamani ya bidhaa zao kwa ajili ya kuuza nje.











Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top