Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga,ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa nyumba 109 za waathirika wa maporomoko ya matope yaliyotokea Desemba 3, 2024 Wilayani Hanang Mkoani Manyara.
Wakati akiweka jiwe hilo amewataka wanufaika wa nyumba hizo kuzitumia vizuri na kuzitunza kwa manufaa yao na vizazi vijavyo viweze kunufaika.
Pia RC Sendiga kwa niaba ya Wananchi wa wilaya ya Hanang' ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajengea nyumba hizo.
Sambamba na hilo, RC Sendiga, ametembelea na kukagua ujenzi wa shule ya Msingi Warret inayojengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 564, Zahanati ya kijiji cha Dawar inayojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 75,000,000., Stendi ya mabasi Katesh inayojengwa kwa shilingi bilioni 5.6 na Kituo cha Afya Gisambalang ambacho kinajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 500.
Akihitimisha ziara yake ya ukaguzi wa miradi hiyo RC Sendiga amewaagiza Viongozi wa wilaya ya Hanang kuhakikisha ujenzi wa miradi hiyo unakamilika ifikapo ama kabla ya tarehe 30 mwezi 12, 2024.





